Sambaza....

Kiungo wa Liverpool Naby Keita amesema anahitaji muda ili kuthibitisha ubora wake na kufidia ada ya uhamisho ya Dollar Milioni 63 ambazo zililipwa kumsajili akitokea RB Leipzig ya Ujerumani.

Keita ambaye ni raia wa Gini ameyasema hayo wakati akihojiwa na Jarida la Klabu ya Liverpool wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur mwishoni mwa Juma hili.

“Nimeambiwa na wengi kuwa wachezaji wengi wanaokuja kwenye Premier League huchukua muda mrefu kuwa na kiwango chao bora, inategemea na hali ilivyo, hivyo kucheza  hapa kunaweza kuwa na ugumu, lakini ninamotisha ya kucheza hapa, sio kwa ajili yangu pekee yangu lakini kwa ajili ya timu nzima na klabu,” amesema.

“Kila mtu ambaye yupo karibu yangu amekuwa akinitia moyo, na mimi hakika natoa kila kitu ili niweze kuzoea mazingira ya hapa haraka iwezekanavyo,” ameongeza.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza kitakachopambana na Tottenham licha ya kuanzia benchi katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Leicester City.

Amekuwa katika shinikizo kubwa kwa sasa kutoka kwa mashabiki na Wachambuzi wa soka ulimwengu, kwani ni Kiungo ambaye amesajiliwa kwa pesa nyingi zaidi katika historia ya Klabu hiyo akitokea RB Leipzig.

“Mimi ni mtu ambaye kama nitafunga mabao nane kwenye msimu mmoja, basi malengo yangu yatakuwa ni kufunga mabao tisa msimu unaofuata, ndivyo fikra zangu zilivyo, EPL ni ligi tofauti na nyingine ambazo nimecheza, lakini nitapambana kwa ajili ya kuvunja rekodi zangu mwenyewe, nina shauku,” amesema.

Sambaza....