Kwenye benchi la ufundi utaangalia uteuzi wa kikosi cha kwanza na manadiliko, mfano kule beki ya kushoto yupo Yasin Mustapha ambaye ni mguu wa kushoto amezidiwa na Kibwana na Faridi? Ni kweli Denis Nkane ndiyo super sub chaguo la kwanza?
Utimamu wa wachezaji upoje? Upo muendelezo kama walivyoanza au imeshuka? Mwalimu wa viungo wa timu ana nafasi ya kutujibia maana hapa kuna kumbukumbu ya miaka yote wanaaanzaga vizuri kule mwishoni huwa ni ‘mustabshilla’.
Wachezaji wanatengeneza nafasi za kufunga au hawatengenezi? Kwa wastani wanapata nafasi za wazi ngapi kwa mechi?, kama jibu ni ndiyo litaongezeka swali zinatumiwa vizuri au hazitumiwi vizuri? Utaona dakika 270 bila nyavu kutikisika hazitumiwi vizuri.
Unadhani kuna mpango wa pamoja toka kwa benchi la ufundi na wachezaji labda wakiwemo na viongozi wa kumwandaa na kumtengenezea Mayele kuibuka mfungaji bora wa msimu?
Au ni mpango wa wachezaji wachache marafiki ndani ya timu kama Feisal Salum alivyotoa ‘lovely pass’ kwa Mayele kwenye sehemu ambayo alipaswa kufunga kwa kupasia nyavu au kushuti ili mchezaji mwingine acheze mpira utakaorudi kama nyanda kacheza.
Kukazia hili na marafiki wachache kumtizama Mayele kama ni mtu anayestahili kuwa mfungaji bora msimu huu ni mazingira ya penati. Licha ya kuamini kwenye mapigo yote ya uwanjani benchi la ufundi huwa linateua mpigaji kutokana na uwezo wake na mazingira yake japo si lazima iwe hivyo.
Lile tukio la Ntibanzokiza kumzuia Djuma Shabani kupiga ile penati na kumpa Mayele lilikuwa na baraka za benchi la ufundi au mtizamo ( uswahiba) wake binafsi?
Mayele ana game ya 3 hajafunga si dhambi wala shaka kwa mshabuliaji yeyote duniani, ila anaondoka kwenye wastani wake wa mechi 2:1 itakapo fika 5/1 kelele zitaanza hakuna mshambuliaji pale 7:1 + kabisaaa aje mwingine.