Sambaza....

Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo imetangaza kuwa aliyekuwa Rais wake Moise Katumbi amerejea katika nafasi yake ya urais wa klabu hiyo baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa akikimbia adhabu ya kifungo kwa sababu za kisiasa. Tovuti ya TP Mazembe imeripotiwa.

Rais mpya wa DR Congo Felix Tshisekedi ambaye amekuwa akihudhuria mechi,ikiwemo ya TP Mazembe na Simba,ametangaza maridhiano ya kisiasa na makundi mbali mbali nchini humo na adhabu ya kifungo cha Katumbi imetenguliwa.

 

Sambaza....