Baada ya tamko la Taasisi ya kumbana na rushwa (TAKUKURU) kusema kua kulikua na matumizi mabaya ya fedha alizotoa Mh. Rais kwaajili ya michuano ya Afcon ya vijana mwaka 2019 na kusema uchunguzi unaendelea na wanaotuhumiwa ni hiari yao kurudisha fedha hizo ama kuruhusu uchunguzi uendelee.
Mkuu wa Takukuru Brigedia John Mbung’o amesema tayari kuna nyaraka zimekusanywa tayari kabisa kwa uchunguzi. Baaya ya kusema hayo wadau wa soka wamekua na maoni tofauti kuhusu tuhuma hizo huku wengi wakitupa lawama kwa TFF moja kwa moja. Lakini leo Rais wa Shirikisho la Soka nchini ametoa maoni yake na kusema anafurahi kuona Takukuru wakifanya kazi yao.
Wallace Karia “Hili swala tayari lipo katika chombo cha serikali nadhani tuliache, si vyema kuliongelea hapa labda nitakua naingilia kazi ya mahakama au uchunguzi lipo kwenye chombo husika.
Lakini pia nimefurahi kwa Takukuru kuingilia hili swala maana nimekua nikituhumiwa na kusemwa kuhusu fedha, nafkiri sasa ukweli utaonekana. Pia mimi nipo tayari hata pia wasaidizi wangu nimewaambia kama tutakua tunahusika tupo tayari kuwajibika.”
Rais Karia pia amesegusia kuhusu fedha za FIFA na kusema wanazielekeza katika kulipa madeni mbalimbali ambayo shirikisha wanayo haswa ya waamuzi wa Ligi zote zilizo chini ya Bodi ya Ligi (TPBL) ambazo ni Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza na la pili.
Wallace Karia ameyaongea hayo alipokua katika mahojiano katika kipindi cha Jaramba cha TBC.