Aliyewahi kuwa golikipa wa Yanga ,Beno Kakolanya amesajiliwa na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
Golikipa huyo aliyevunja mkataba wake na Yanga kutokana na kutomaliziwa pesa zake za usajili, hali hii ilimfanya agomee mazoezi na Yanga.
Baada ya kugomea mazoezi ya Yanga, kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema hamwihitaji tena kipa huyo ndani ya kikosi chake.