Kaizer Chiefs iko tayari kukubaliana na ombi la mkufunzi Nasreddine Nabi kuwaleta wasaidizi wake anaowataka kuambatana nao, SABC Sport imesema.
Amakhosi wameamua kumtafuta kocha mwingine katika nafasi ya kocha wao Arthur Zwane ambaye hakufanya vyema katika msimu uliomalizika. Kocha Nabi raia wa Tunisia bado ndiye anayelengwa na klabu hiyo kuwania kiti hicho.
Kama ilivyoripotiwa hivi majuzi na shirika moja la utangazaji , Kaizer Chiefs wamekaa vikao kuhusu Nabii mara kwa mara katika mikutano ili kujadili mustakabali wake na wababe hao wa Soweto ungekuwaje iwapo atakubali kuchukua nafasi hiyo.
Nabi yupo tayari kwenda Kaizer baada ya kukataa mkataba mpya na Young Africans ya Tanzania, ambapo alishinda mataji sita ndani ya miaka miwili na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF mwezi uliopita.
Hili ndio lililowavutia Chiefs na kujaribu kumbana Nabi ili kuhamiz Ligi Kuu ya Soka (PSL), lakini kumekuwa na kikwazo kwake kwa benchi lake la ufundi Chiefs awali walitaka Zwane bado awe sehemu yake.
Kulingana na vyanzo, Chiefs sasa wamemwambia Nabi kwamba anaweza kuleta hadi wasaidizi wake wawili na wanamwachia kocha kuamua katika idara gani. Amakhosi bado wana Dillon Sheppard mwenye kandarasi ya mwaka mmoja zaidi na watahitaji kuthibitisha jukumu lake jipya iwapo Nabi atateuliwa.
Sheppard alijiunga na Chiefs Septemba 2021 kama kocha msaidizi wa Gavin Hunt na alishika nafasi hiyo hiyo wakati Zwane alipoinuliwa na kupewa timu ya kwanza.
Kuna tetesi huenda kwamba mazungumzo ya hivi karibuni yanaweza kuwaleta Amakhosi karibu na kukubaliana juu ya masharti na Nabi kabla ya kikosi kurejea kwa ajili ya maandalizi ya msimu na pia kabla ya uzinduzi wa jezi mpya na kampuni ya Kappa. Lakini kama Nabi anahisi vivyo hivyo, kwa vile sasa anatakiwa kuafikiana na kuzingatia ni nani atamchagua kujiunga naye Afrika Kusini.