Sambaza....

Kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) Mshami Vincent amewaita wachezaji 27 wa kuunda kikosi cha awali cha timu hiyo kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwenye fainali za mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Ivory Coast mjini Abidjan.

Katika kikosi hicho mchezaji pekee anayecheza ligi kuu Tanzania Bara Meddie Kagere (mshambuliaji wa Simba SC) ndiye aliyejumuishwa wakati wachezaji wengine akiwemo nahodha wa zamani wa Amavubi na kiungo na Simba Haruna Niyonzima wakiachwa.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na washambuliaji Kagere Meddie (SC Simba, Tanzania), Tuyisenge Jacques (Gor Mahia, Kenya), Hakizimana Muhadjiri (APR FC), Nshuti Dominique Savio (APR FC), Nizeyimana Juma (Kiyovu Sports), Byiringiro Lague (APR FC) na Iradukunda Bertrand (Mukura VS&L)

Viungo ni Butera Andrew (APR FC), Niyonzima Ally (APR FC), Muhire Kevin (El Dakhleya Sporting Club, Egypt), Niyonzima Olivier (Rayon Sports FC), Nsabimana Eric (AS Kigali), Bizimana Djihad (Waasland Beveren, Belgium) and Nshimiyimana Imran (APR FC), Imanishimwe Emmanuel (APR FC), Habimana Hussein (Rayons Sports FC), Iragire Saidi (Mukura VS&L), Rutanga Eric (Rayon Sports FC) na Iradukunda Eric (Rayon sports FC).

Walinzi yupo Rwatubyaye Abdoul (Sporting KC, USA), Nirisarike Salomon (FC Tubize, Belgium), Manzi Thierry (Rayon Sports FC), Buregeya Prince (APR FC) na Fitina Ombolenga (APR FC),

Wakati walinda mlango ni Rwabugiri Omar (Mukura VS&L), Kimenyi Yves (APR FC) na Mvuyekure Emery (Tusker FC, Kenya).

Kikosi hicho kitaingia kambini Machi 14 na kufanya mazoezi ya kawaida hadi March 20 ambapo Machi 21 watasafiri kuelekea Ivory Coast kukamilisha mchezo huo wa mwisho wa kundi H , mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba kwani tayari Ivory Coast na Guinea washafuzu kushiriki AFCON itakayofanyika nchini Misri mwezi Juni.

“Tunajua tumetoka kwenye mashindano haya kwa kuwa hatuna nafasi ya kusonga mbele, lakini hili halituumizi kichwa, tutapambana kulinda heshima, na itakuwa fursa kwa ajili ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani kuonesha uwezo wao,” Kocha Vincent amesema wakati akitaja majina hayo.

Sambaza....