Nyota Mnyarwanda na mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ni kama anatafuta kuivunja ratiba yake mwenyewe katika ufungaji wa mabao katika Ligi Kuu Bara.
Iko hivi Meddie Kagere katika msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Bara akiwa Simba sc alifunga mabao 23 yaliyotosha kumfanya kuwa mfungaji bora wa Ligi mbele ya Salim Aiyee (Aliekua Mwadui fc) na Heritier Makambo (Aliekua Yangasc).
Baada ya msimu kumalizika na kuibuka Galacha wa mabao kwa mabao yake 23 msimu huo wa 2018/2019 Meddie Kagere alikabidhiwa tuzo yake ya ufungaji bora na tovuti ya Kandanda.co.tz
Kwa msimu huu tayari Meddie Kagere ana mabao 21 huku kukiwa na michezo miwili imebaki kuelekea kumalizia Ligi Kuu Bara. Kwa magoli yake 21 yanamfanya kuwa kinara wa ufungaji mpaka sasa huku akifwatiwa na wazawa Yusuph Mhilu na Leriant Lusajo.
Tazama hapa chati ya ufungaji mabao mwa msimu huu.
Ikiwa Meddie Kagere atafanikiwa kufunga mabao mawili na kufikisha mabao 23 basi atakua amevunja rekodi yake mwenyewe ya msimu uliopita ya mabao 22. Lakini pia endapo atafanikiwa kufunga bao moja atakua amefikia rekodi yake pia ya msimu uliopita ya mabao 22.
Simba imebakiwa na michezo miwili ya ugenini kanda ya Kaskazini ambapo itacheza na Coastal Union Mkwakwani na kumalizia Ligi katika dima la Ushirika Moshi dhidi ya Polisi Tanzania.