Sambaza....

Hatua ya kwanza ya kufuzu kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022 kwa nchi za Afrika imeshamilika huku Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Rwanda, Meddie Kagere aongoza kwa kupachika mabao.

Rwanda imefuzu hatua ya makundi kama ilivyo kwa Tanzania kwa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Seychelles. Kagere alifunga bao moja katika mechi ya kwanza ugenini katika ushindi wa goli 3-0, mechi ya pili nchini Rwanda, Kagere alifunga mabao mawili katika ushindi wa goli 7-0.

Meddie Kagere

Katua hatua ya kwanza, iliyoshirikisha timu 28 zenye viwango vya chini kwa mujibu wa FIFA zilikutana ili kutoa timu 14 zitakazokutana na timu 26 zenye viwangoi vya juu zaidi kuunda timu 40 zitakazoingia katika hatua ya makundi. Katika hatua hii  magoli 57 yamefungwa  katika mechi 28 ikiwa ni wastani wa goli 2.04 kwa kila mechi.

Kagere yupo kileleni akiwa na goli 3 wakiungana na Ramadan Agab wa Sudan na Joseph Mendes wa Guinea-Bissau. Wengine ni Yannick Mukunzi, Jacques Tuyisenge, Muhadjiri Hakizimana wote kutoka Rwanda na Peter Shalulile wa Namibia wakiwa na magoli mawili kila mmoja.

Hatua ya kwanza imeshamalizika, hatua ya pili ndiyo inayofuata. Hatua hii itahusisha timu 14 washindi wa hatua ya kwanza na timu 26 zenye viwango vya juu kuunda timu 40 zitakazopangwa katika makundi 10 yenye timu 4 kila moja. Kisha atakayeongoza kundi atasonga hatua ya tatu nay a mwisho ambapo timu 10 hucheza mechi mbili za mtoano kupata timu 5 zitakazoiwakilisha Afrika katika kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Timu 14 zilizofuzu hatua ya kwanza ni Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Angola, Guinea-Bissau, Malawi, Togo, Sudan, Rwanda, Tanzania, Equitorial Guinea, Ethiopia, Liberia na Djibouti.

Sambaza....