Ligi kuu ya soka Tanzania bara iliendelea leo, kwa mchezo mmoja kupigwa kule Bukoba mkoani Kagera kunako dimba la Kaitba
Katika mchezo ambao ulizikutanisha klabu za Kagera Sugar waliowakaribisha waoka mikate Azam FC ambapo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1
Kwa matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuifikisha alama 34, na kulingana kwa alama na mabingwa watetezi Yanga ambao wana mchezo mmoja mkononi
Kagera sugar wanafikisha alama 14, wakilingana alama na Njombe FC lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo Kagera sugar wakisogea kunako nafasi ya 15
Katika mchezo wa leo Kagera sugar ndio walikuwa wa kwanza kupata bao, kupitia kwa beki wake Edislaus Mfulebe kunako dakika ya 53, kabla ya dakika chache baadae Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC
Kagera sugar waliwakilishwa na Ramadhan Mohammed, Mwaita Gereza, Edslaus Mfulebe, Juma Shemvuni, Mohammed Faki, George Kavila/Peter Mwaliyanzi dk 55, Suleiman Mangoma, Ally Nassor, Jaffary Kibaya/ Edward Christopher dk 77, Ally Ramadhan na Venance Ludovick/ Atupele Green dk 70
Azam FC Razack Abarola, Saleh Abdallah/ Iddi kipagwile dk 46, Bruce Kangwa, David Mwantika, Yakub Mohammed, Stephen Kingue/ Paul Peter dk 73, Abdallah Kheri, Frank Domayo, Salmin Hoza, Mbaraka Yusuf/Enock Atta dk 46, na Shaban Iddi Chilunda
Ligi hiyo inataraji kuendelea tena Jumatano, ambapo mabingwa watetezi Yanga sc wataikaribisha Majimaji FC kunako dimba la Uhuru, Dar es salaam, huku Simba sc ikiivaa Mwadui FC siku ya Alhamis kunako la CCM Kambarage mkoani Shinyanga
Ikumbukwe kuwa michezo hiyo ni ya viporo, ambapo ilitakiwa kuchezwa mwishoni mwa juma lililopita lakini vigogo hao walikuwa na michezo ya kimataifa