Sambaza....

Mlinda Mlango Ramadhan Kabwili amepangwa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ kinachoshuka usiku huu kucheza na timu ya Vijana ya Mali.

Kabwili ambaye hakucheza katika mchezo wa kwanza Ngorongoro wakikubali kichapo cha mabao 2-1 jijini Dar es Salaam, amepangwa kuanza huku kipa aliyedunguliwa mabao hayo Abdutwalib Mshery akianzia benchi.

Aidha mshambuliaji wa Mbao FC Habibu Haji Kyombo kwa mara nyingine tena katika michezo mitatu mfululizo ataanza huku winga wa Yanga Said Bakari ‘Ronaldo’ naye akipata nafasi ya kuanza wakati Issa Makamba na Asad Juma wakianzia Benchi.

Kikosi Kamili: Ramadhan Kabwili, Kibwana Shomari, Hance Msonga, Dickson Job, Enrick Nkosi, Shaban Ada, Kelvin Nashon, Paul Peter, Habibu Kyombo na Said Bakari.

Akiba: Abdutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Ally Ng’anzi, Hamis Abdul, Muhsin Makame, Issa Makamba, Israel Mwenda, Daud Nasry na Asad Juma.

Ngorongoro Heroes Itajitupa Uwanjani Majira Ya Saa Mbili Kamili Usiku Huu Kwa Saa Za Afrika Mashariki Kucheza Na Mali Katika Mchezo Wa Duru Ya Pili Kuwania Nafasi Ya Kucheza Fainali Za Mataifa Afrika Kwa Vijana Mwakani Nchini Niger.

Vijana Hao Watahitaji Kupata Ushindi Wa Kuanzia Mabao Mawili Kwa Sifuri Ili Kujihakikishia Kufuzu Katika Hatua Inayofuata Ambapo Watakutana Na Cameroon Waliowatoa Uganda.

Mchezo Huo Utapigwa Katika Uwanja Wa Modibo Keita Mjini Bamako.

Sambaza....