Sambaza....

 

Mwaka 2015 ndiyo mwaka rasmi uliompa uhuru Jurgen Klopp kuja katika klabu ya Liverpool. Klabu yenye walevi wa mpira wa miguu na bila shaka walipatana kwa sababu na yeye ni mlevi wa mpira wa miguu.

Tangu mwaka 2015 , ni msimu wa mwaka 2018/2019 uliompa uwezo Jurgen Klopp kuipa ubingwa Liverpool. Ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mwezi wa sita mwaka huu na mwezi wa nane mwaka huu aliipa ubingwa wa supercup.

 

Awali Jurgen Klopp alifanikiwa kuifikisha Liverpool katika fainali ya Europa League. Na msimu huu anaongoza ligi kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya Leicester City ya Brendan Rogders kocha wa zamani wa Liverpool.

Brendan Rodgers alikaribia kuipa ubingwa Liverpool, kosa la nahodha Steven Gerrald mbele ya Chelsea liliwanyima ubingwa wa kwanza tangu 1990. Leo hii Jurgen Klopp anaonesha dalili ya kuwapa ubingwa Liverpool na Liverpool wamempa mkataba mpya utakaomfunga mpaka mwaka 2024.

Sambaza....