Mlinda mlango namba moja wa Timu ya Taifa na KMC Juma Kaseja “Tanzania one” ameongea mengi alipokua akiongea na waandishi wa redio ya EFM katika kipindi cha michezo cha Sports Headquotar.
Juma Kaseja amesema moja ya mechi ambayo hatoisahau ni mchezo wa Simba na Zamalek iliyopigwa Cairo Misri mwaka 2003, huku pia akifichua jinsi viongozi walivyofanya kazi kubwa kufanikisha ushindi katika mchezo ule.
Juma Kaseja ” Katika michezo kama ile viongozi hugeuka wafanyakazi na sisi wachezaji tunakua mabosi, ndugu yangu Aveva anaijua hili alikua anafanya kila kitu wakati kama huu.
Nilikua nikimtuma maji analeta, lete juice analeta na ikifika kipindi cha kupasha misuli sisi wachezaji tujaenda uwanjani wao wanabaki kulinda vyumba. Walikua wanafanya yote haya kwa usahihi kabisa.”
Kaseja pia alizungumzia mchezo huo kama moja ya mechi ngumu sana kwake kucheza akisema ndio mchezo ambao hatokuja kuusahau maishani mwake.
Kaseja “Ndio ulikua mwaka wangu wa kwanza Simba mchezo wa kwanza tulishinda moja bila hapa Tanzania halafu tukaenda Misri. Walee jamaa walitushambulia sana lakini mwisho wa siku Mungu ndie aliepanga tuibuke na ushindu siku ile”
Katika mchezo huo Simba ilifanikiwa kuitoa Zamalek kwa mikwaju ya matuta na kuingia robo fainali ya klabu bingwa Afrika.