Sambaza....

Ligi Kuu inaendelea tena hapo kesho ambapo michezo miwili itapigwa huku mchezo wa mapema saa kumi utakua ni kati ya wenyeji KMC watawakaribisha Singida Big Stars katika Uwanja wa Uhuru majira ya saa kumi jioni.

KMC inashika nafasi ya 14 wakiwa kwenye hatari yakucheza michezo ya Playoffs wakati Big Stara wao wapo nafasi ya 4, kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa KMC Julio Kihwelo amesema “Nashukuru sasa timu yangu imeshaingia kwenye mfumo kwasababu wachezaji wangu yale niliyowalekeza kwaajili ya michezo yetu iliyobaki inaonekana wameyashika na wanajua majukumu yao.” 

Kocha huyo atakaesimama katika benchi la KMC kwa mara ya pili akichukua mikoba ya Hitimana Thiery amekiri ugumu wa Ligi hiyo lakino amesema watapambana mpaka mwisho na kuibakisha timu Ligi Kuu.

Kikosi cha KMC

“Mechi za Ligi kuu ni ngumu na ndio maana timu zote zilizo chini ya nafasi ya kumi lolote linaweza kutokea, tumejipanga vizuri ili kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars,” alisema Julio na kuongeza

“Tunajua tunakwenda kucheza dhidi ya timu ngumu ya Singida, ingawa tayari timu nne za kuiwakilisha nchi zimeshajulikana Simba, Yanga, Azam na Singida lakini najua wao watataka heshima zaidi ili washinde waweze kusogea juu nafasi ya tatu, sisi tupo nafasi ya 14 lakini tunapambana ili tutoke huku chini tusishuke daraja mwakani tuwepo Ligi Kuu.”

Katika mchezo wa kesho KMC watawakosa nyota wake  Matheo Anthony ambae ni majeruhi, Andrew Chikupe na Baraka Majogoro wenye kadi tatu za njano.

Sambaza....