Wachezaji wawili wa Klabu ya Simba kiungo Jonas Gerald Mkunde na Habibu Kyombo huenda wakawa miongoni mwa wachezaji wakwanza kuondoka na kuelekea nchini Ulaya katika usajili huu utakaoanza hivi karibuni.
Jonas Mkude na Habibu Kyombo wanaweza wakawa wachezaji wakwanza kunufaika na mpango wa ushirikiano kati ya Klabu yao ya Simba na Western Armenia ya nchini Armenia uliotangazwa hivi karibuni.
Wawili hao baada ya mchezo wamwisho wa ligi kumalizika dhidi ya Coastal Union walionekana kuwa na kikao kirefu na Mtendaji wa Simba Sc Imani Kajula, Rais wa Western Armenia Andrenick Martirosyan pamoja na maofisa wengine wa klabu hiyo.
Kikao hicho kilidumu takribani dakika 15 huku wote wachezaji, mtendaji wa Simba na viongozi wa Western Armenia wakionekana kuchangia maongezi hayo.
Wawili hao wamekua hawapati nafasi katika klabu ya Simba hivi karibuni na tetesi zikisambaa huenda waachwa na Simba kuelekea msimu ujao. Jonas akitajwa kuhusishwa na Singida Big Stars wakati bado Habibu haijafahamika atatimkia wapi.
Kupitia taarifa ya Simba ikitangaza uhusiano na klabu hiyo ilisema “Klabu yetu leo imeingia mkataba wa ushirikiano na Western Armenia Football Club inayoshiriki Ligi Kuu ya Armenia, Ulaya ya Mashariki.
makubaliano ya ushirkiano huo yatakuwa kwenye maeneo makubwa manne, Kiufundi, Ubadilishanaji na uuzianaji wa wachezaji, Soka la vijana na mafunzo kwa wakufunzi.”
Hivyo huenda Jonas Mkude na Habibu Kyombo wakwa wakwanza kuhusika katika mabadilishano ya wachezaji baina ya timu hizo. Jonas Mkude ana zaidi ya miaka 10 na Simba wakati Habibu ndio kwanza amemaliza msimu na Simba, akiwa na mwaka mmoje pekee.
Baada ya kikao hicho Kandanda.co.tz iliwatafutawachezaji wote wawili hao kuelezea kikao hicho lakini hawakua tayari kuzungumza.