Wapwa, mara nyingi nimekuwa nikisema kuhusiana na timu nyingi za Ligi Kuu hususani za mikoani kuwaogopa sana timu za Kariakoo wanapocheza nazo.
Waweza kusema zina mchecheto au ‘mapepe ‘ hivyo hufanya makosa mengi sana wakiwa uwanjani yanayowanufaisha wakubwa hawa kutoka Kariakoo.
Hivyo hata kujua udhaifu wa mtu moja moja toka kwa wakubwa ni ngumu sana ila wakienda Kimataifa kwa wakubwa wenzao unaona hayo mapungufu hayo katika mechi zao wanazocheza.
Mfano ukimuangalia Joash Onyango moja wa walinzi wa kati bora kabisa miaka kadhaa nyuma utakubaliana nami katika hili.
Akiwa kwenye michuano ya kimataifa si anakuwa si huyu unaweza kumkataa katakata, lakini anapokuwa hapa kwenye ligi na mashindano ya ndani shughuli yake utaiona haswa.
Atapiga ma takling ya kufa mtu atageuka pande zote ndani ya box mara kulia mara kushoto kama kiungo vile. Atatoa mpira kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa ufundi mkubwa huku akiringa kulia kushoto kama ambavyo alifanya kwenye mchezo wa Namungo.
Shughuli inakuja kule kwa wajanja wenzetu wa juu zaidi’ intensity’ ya mchezo huwa inaenda kuwa juu yake kasi na kujiamini huwa vinamuelemea na kupoteza kabisa uwezo wake.
Madhara yake kuonekana kwenye makosa makubwa( kutoa maboko ) yanayoigharimu timu kama katika michezo miwili dhidi ya Wydad na Raja Casablanca katika Ligi ya Mabingwa.
Sijui kama ulifuatilia vizuri katika mchezo dhidi ya Namungo na siku nyingine katika michezo ya Ligi na kisha ukarudi kukumbuka mechi za Ligi ya Mabingwa ama Kombe la Shirikisho.