The MVP is here! Hapa ndipo ulipo umiliki wa eneo la Kiungo ukipenda hata eneo la ulinzi. Ndio huyu MVP wa Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa Mwaka 2021-22.
Yes! Ni Yanick Litombo Bangala wengi wanapenda kumuita “Mzee wa kazi chafu” ukimpa pasi mbaya atakuletea nzuri ukipenda afanye kazi ngumu kuwa rahisi atafanya. Sehemu zenye vurugu atapeleka usalama
Pale Young Africans alitumika kama kiungo mkabaji lakini pia mlinzi wa kati, kocha mkuu wa Wananchii wakati ule Mohamed Nabi alihitaji mfumo wake uwe na Yanick Bangala ili timu iwe na uhai kwenye uzuiaji.
Ni ngumu sana kuzungumza kuhusu Young Africans wakati ule pasipo Yanick Bangala lakini sasa imekuwa hivyo. Jezi yake kwa sasa sio njano na kijani bali ni bluu na nyeupe pale Azam Complex, Dar Es Salaam.
Hii sio stori ya mchezaji tu bali ni simulizi kuhusu Mchezaji Bora wa Ligi Kuu! Ooh no let me write in English “The Most Valuable Player” of the Year 2021-22! Simply, pale Azam FC watapata burudani yake
Inavutia sana, nyuma ya Feisal Salum na James Akaminko atacheza Yanick Bangala. Naiona Azam FC imara kwenye eneo la kiungo mbele ya watu hawa watatu endapo watakuwa katika ubora wao.
Pale Young Africans amewapa makombe ya Ligi Kuu, ASFC, Ngao ya Jamii na Fainali ya CAF CC hii inatosha sana kwake kusema ameacha alama kubwa Jangwani. Jezi ya njano na kijani imevuja ameipa heshima kubwa sana alipokuwa uwanjani
Chamanzi wamekusajili ukawapa burudani! Wameona Jezi ya Blue na Nyeupe inapendeza na ni sahihi sana kwako ukiwa ndani ya Uwanja. Fahamu tu kwamba Azam FC inataka kushinda Makombe ambayo wameyatafuta kwa muda mrefu sana
Yanick Bangala fahamu kwamba mara ya mwisho Azam FC kushinda Ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa Mwaka 2014 na wanaamini Mwaka 2024 watachukua Ubingwa mwingine, achilia mbali ASFC ambayo wanahitaji na Kufanya vizuri Kimataifa.
Wao wanasema Timuborabidhaabora hivyo nenda kawape kiwango bora na washinde makombe Bora kwa kiwango bora uwanjani. Mashabiki wanasubiri kuona ukifanya makubwa ndani ya Jezi yao!. Let’s Enjoy the beautiful football.