Sambaza....

Ligi Kuu ya NBC imeendelea kushika kasi huku ikielekea hatua za lala salama ushindani ukiongezeka kwa vilabu vyote  vinavyoshiriki Ligi hiyo. Wapo wanaopambania kushuka daraja, wanaowania nafasi za kimataifa na wanaogombea ubingwa.

Kutokana na ushindani huo umepelekea kuwekwa kwa rekodi mbalimbali na kunogesha ligi hiyo ambayo ni namba tano kwa ubora barani Afrika.

 

Miongo mwa rekodi ya kuvutia zaidi ni rekodi ya goli la mapema zaidi kufungwa katika mchezo mchezo wa Ligi hiyo. Na rekodi hiyo inashikiliwa na Prince Dube wa Azam Fc kwa goli lake alilowafunga Simba katika mchezo wa raundi ya pili wa Ligi uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Dube alitumia sekunde 15 pekee tangu mpira kuanza kumtungua Aishi Manula baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa James Akamiko na kuwa bao la haraka zaidi miongoni mwa mabao sita ya haraka yaliyofungwa msimu huu mpaka sasa.

Nickson Kibabage

Bao la pili la haraka zaidi limefungwa na Nickson Kibabage akiwa na Mtibwa Sugar alipowafunga Mbeya City katika sekunde ya 58. Goli la Ismail Mgunda lililofungwa dakika ya kwanza limeshika nafasi ya tatu katika orodha hiyo.

Moses Phiri “Jenerali” anashika nafasi ya nne kwa wachezaji waliofunga bao la haraka zaidi kwa goli lake alilowafunga KMC katika mchezo wapili wa Ligi msimu huu. Goli hilo Priri alilifunga dakika ya pili ya mchezo.

Moses Phiri.

Nafasi ya tano imeshikiliwa na wachezaji wawili ambao wamefunga katika dakika ya tatu. Alli Kipemba alifunga bao katika mchezo dhidi ya KMC na Matheo Anthony dhidi ya Ihefu.

Sambaza....