Kocha mpya wa Yanga sc, Mwinyi Zahera, amelazimika kubadili mavazi ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza rasmi kukinoa kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
Siku ya kwanza alipoanza kukinoa kikosi hicho kilichopiga kambi mjini Morogoro, alionekana akiwa amevalia jezi yenye rangi nyekundu ambayo hutumiwa na mahasimu wao Simbasc, jambo ambalo lilionekana kuwakera mashabiki wa Yanga
Kwa Zahera, alikuwa tatizo kwake kwa maana ni jezi ya timu ya taifa lake DRC Congo ambapo sehemu ya jezi hizo huwa na rangi nyekundu kama utambulisho wa bendera yao
Aidha katika kile kinachoonekana kuwa Uongozi wa Yanga sc sio wa mchezo mchezo, jana ulimbadilishia jezi kocha kocha huyo ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kukinoa kikosi chao
Gumzo kuhusiana na kocha huyo, lilizuka baada kutua nchini akiwa amevaa suti iliyoambatana na tai ya rangi nyekundu hali iliyopelekea mashabiki wa Simba sc kuwatambia wale Yanga kuwa kocha huyo ana damu ya Msimbazi
Zahera, amechukua nafasi ya kocha George Lwandamina aliyetimka klabuni hapo mwanzoni mwa mwezi huu.