Katika mchezo wa mpira wa miguu jezi namba moja inajulikana kwa matumizi ya mlinda mlango awapo uwanjani. Imezoeleka na ipo hivyo kuwa kila wakati anaevaa namba moja ndie mlinda mlango wa timu.
Ingawa huwa kuna kipa namba mbili ambao hulazimika kuvaa namba nyingine katika jezi yake. Katika Ligi Kuu Bara walinda mlango wengi wamekua wakipendelea kuvaa jezi namba 30 mara nyingi.
Walinda lango wa timu nyingi za Ligi Kuu Bara msimu huu wanaopata nafasi za kuanza katika vikosi vya kwanza katika vilabu vyao wamekua wakivaa zenye namba zingine tofauti na namba moja migongoni mwao.
Ni kama jezi namba moja haina soko vile kwa makipa wa VPL hii ni kutokana na kua magolikipa wengi wanaovaa namba hiyo wanasugua benchi katika timu zao.
Jinsi ambavyo namba moja ina gundu katika timu mbalimbali za VPL:
SimbaSc – Aishi Manula 28
Ndio kipa namba moja wa Simba kwa sasa huku akimuweka benchi Said Mohamed Nduda anaevaa jezi namba moja. Huku Said Mohamed akiambulia kudaka mechi mbili tu za VPL za kukamilisha ratiba.
AzamFc – Razack Abarola 16
Anamuweka kwenye benchi kipa mkongwe Mwadini Ally ambae ndie anaivaa jezi namba moja pale Chamanzi Complex baada ya kushindwa kuziba pengo la Aish Manula alieenda Simba.
Singida utd – Manyika Jnr 18
Amefanikiwa kumzidi kete Ally Mustapha “Bartez” na Said Lubawa kufanikiwa kuwa kipa namba moja hivyo kuiweka jezi namba moja benchi na kutambaa chini ya kocha Hans Plujim.
YangaSc – Youth Rostand 30
Alitoka African Lyon na kutua Yanga nakufanikiwa kua kipa namba moja na kumueka Kabwili kama msaidizi wake ambae ndie kipa anaevaa jezi namba moja.
Mtibwa Sugar -Benedict Tinocco 18.
Abdallah “Dida” na Shabani Kado wameshindwa kufua dafu na kumuacha Tinoco akikaa golini, huku jezi namba moja ikivaliwa na Abdallah Dida ambae muda mwingi amekaa bechi.
Tanzania Prisons – Aron Kalambo 18.
Kipa aliedaka michezo mingi katika VPL nyuma ya Aishi Manula na kuweza kuisaidia kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara msimu huu.