Klabu ya Simba hapo jana rasmi ilimtambulisha Mikael Igendia kuwa meneja wake mpya na mkuu wa Sayansi ya michezo ili kuchukua nafasi ya Patrick Rweyemamu aliyehamishiwa kwa vijana.
Kupitia taarifa rasmi ya klabu Simba imesema “Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri Mikael Igendia raia wa Kenya kuwa Meneja wa timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo kwa mkataba wa miaka miwili.
Igendia (36) anachukua nafasi ya Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa Mkuu wa Programu za soka la vijana.”
Mchambuzi wa soka na meneja wa zamani wa Azam Fc Jemedary Said ameuchambua wasifu wa Igendia na kumuelezea faida zake. Jemedary Said ameandika hivi:
Ni kijana mdogo mwenye ujuzi katika usomi usitie shaka ana (Bachelor’s and Master’s). Ana shahada katika Sayansi ya Michezo wanasema Sports Science alizopata nchini Finland hii inajumuisha Analyst na Utawala.
Pia ni Certified Sports Masseur yaani mchua misuli aliesomea katika Academy ya Carl Wihelm – Finland na kumalizia kazi ujuzi wake kwa mafunzo katika timu ya AFC Bournemouth nchini England na kuwa Strength and Conditioning Coach yaani Mtaalam wa utimamu wa mwili.
Katika kazi ana uzoefu katika Timu za Wanariadha, timu za Michezo ya mbio za magari na timu za mpira ambapo hapa kwenye soka alikuwa na timu ya Gor Mahia na Timu za Taifa ya Kenya mbalimbali za kike na kiume za vijana na wakubwa kwa muda tofauti pia hivi karibuni mwaka huu 2023 aliazimwa kwa muda maalum Taifa Stars wakati wa mechi dhidi ya Uganda zote mbili.
Mikael Igendia, ameajiriwa Simba kama timu meneja kutokana na uzoefu wake wa utawala aliosomea ila aliishi nao kufanyia kazi, pili ameajiriwa Simba kuwa Performance Analyst kwasababu ana elimu kubwa ya Sayansi ya Michezo pia ameajiriwa Simba sababu ni mtaalam wa utimamu wa mwili kama Mkuu wa wachua misuli aliekamilika hivyo kuitwa Meneja wa Timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo imejumuisha mambo yote hayo ukipenda unaweza kusema Strength and Conditioning Coach.
Hivyo Igendia yupo Simba kutokana na uzoefu wake na elimu yake yenye uzoefu na mchanganyiko wa mambo mengi kwa wakati mmoja kwa mtu mmoja huku akiweza kuongea lugha mbalimbali hii itaboresha benchi la ufundi kwa kiasi kikubwa ndio matumaini ya Waajiri kutoka kwake.