Sambaza....

Timu ya Simba sc leo imecheza mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwenye uwanja wake wa nyumbani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuweka hai ndoto yake yakufika nusu fainali.

Mchezo huo umemalizika kwa Simba sc kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila goli hilo likifungwa na mshambuliaji raia wa Congo Jean Baleke dakika ya 30 pasi ya usaidizi ikipigwa na Kibu Denis  Prospar.

Kocha wa Simba sc Mbaziri Robetinho ameisifu timu yake nakusema ”Tulicheza kipindi cha kwanza kwa mpango mwingine na kipindi cha pili tulibadili namna ya uchezaji wetu tulimsogeza juu Chama kwenye kushambulia na tukamrudisha Kibu Denis kwenye eneo la kiungo.”

Jean Baleke akifunga bao pekee la Simba katima mchezo huo mbele ya walinzi wa Wydad Casablanca

Lakini kwa upande wa kocha Wydad alionekana kama kutokubaliana na maamuzi ya refa wa mchezo huo na atajiandaa na mchezo ujao ili ashinde na kusonga mbele hatua inayofuata.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa nchini  Morocco katika Jiji la Casablanca siku ya Jumamosi saa nne usiku kwa saa za Tanzania huku Simba ikihitaji sare ili kuvuka kwenda nusu fainali.


Sambaza....