Ligi kuu ya England imemalizika leo kwa kushuhudia Liverpool kubeba imebeba taji lake la kwanza baada ya miaka 30 , wakati huo huo timu nne ambazo zimefanikiwa kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao ni Liverpool, Manchester City , Manchester United na Chelsea.
Kwenye tamati hii ya ligi kuu tumeshuhudia mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy akichukua kiatu cha ufungaji bora baada ya kumaliza wa kwanza kwenye mbio za ufungaji bora.
Jamie Vardy amewazidi Dany Ings pamoja na Pierre-Emirck Aubameyang ambao wote kwa pamoja wamemaliza ligi kuu ya England wakiwa na magoli 22 , goli moja nyuma ya Jamie Vardy.
Jamie Vardy avunja rekodi ya Didier Drogba iliyowekwa msimu wa mwaka 2009/2010 ambapo Didier Drogba aliibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 29 na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora aliyefunga kwenye umri mkubwa , wakati huo alikuwa na miaka 32.
Jamie Vardy amekuwa mfungaji bora msimu huu akiwa na umri wa miaka 33 . Wafungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita Saido Mane na Mohammed Salah wameshindwa kuwika msimu huu mara baada ya kumaliza wakiwa na magoli 18 kwa Saido Mane na goli 19 kwa Mohammed Salah.