Sambaza....

Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imeachana na wachezaji sita (6) akiwemo James Kotei. James Kotei alisajiliwa na Kaizer Chiefs msimu huu akitokea kwenye klabu ya Simba ya Tanzania.

Baada ya kuachana na Kaizer Chiefs kuna tetesi kuwa klabu ya Simba inampango wa kumrudisha katika timu hiyo. Taarifa za ndani zinaonesha kuwa viongozi wa Simba wanataka kumrudisha kiungo huyo.

Kotei (Kushoto)

Baada ya kuonekana katika kikosi cha Simba eneo la kiungo cha kuzuia lina matatizo kidogo kutokana na pengo la James Kotei, hivo wanaona James Kotei ndiye mtu sahihi wa kumrudisha kwenye nafasi hiyo.

Sambaza....