Uongozi wa Yanga sc, umemshusha nchini kocha Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemoklasia ya Kongo, kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo
Taarifa kutoka klabuni hapo, zinasema kuwa kocha huyo ataondoka kesho jijini Dar es salaam kwenda Morogoro ambako kikosi cha timu hiyo kimeweka kambi kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi mahasimu wao Simba sc
Mwinyi, ambaye alikuwa kocha msaidizi kunako timu ya taifa ya Kongo DRC, The Leopards tangu Septemba 30, mwaka jana lakini pia alivifundisha vilabu kadhaa vya Ulaya na nchini kwao Kongo DRC
Kocha huyo ameifundisha DC Motema Pembe ya DRC kuanzia Machi 1, 2015 hadi Machi 10, 2016 akitoka kuinoa FC Tubize ya Ubeligiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, 2014 alijiunga nayo akitoka kuwa Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC
Zahera Mwinyi alizaliwa Oktoba 19, 1962 alianza kucheza soka mwaka 1975 kunako klabu ya Bankin ya Goma, kaskazini mwa jimbo la Kivu hadi mwaka 1980, na ana leseni A ya Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA)
Kocha huyo, anachukuwa nafasi ya George Lwandamina aliyetimka klabuni hapo wiki mbili zilizopita, na kujiunga na timu yake ya zamani ya Zesco United