Sambaza....

Michuano ya Sportpesa Super Cup imezidi kunoga na kushika kasi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya hatua ya robo fainali kuhitimishwa leo Taifa “Kwamchina” .

Baada ya jana kuonekana ni siku ya Wakenya katika robo fainali ya Sportpesa super cup baada ya timu za Kariobangi Sharks na Bandari fc za Kenya kuwasukuma nje ya mashindano Singida United na Yanga sc. Lakini leo imekua kinyume baada ya Watanzania kuzinduka na kulipa kisasi baada ya Simba kuitupa nje AFC Leopard na Mbao Fc kuwabwaga mabingwa watetezi Gor Mahia.

Davis Mwassa nahodha wa Mbao fc akijiandaa kupiga tuta.

Kwa matokeo hayo yanaifanya ratiba ya Sportpesa Supercup ya nusu fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa kuzikutanisha timu za Tanzania dhidi ya Kenya.

Siku ya Ijumaa Simba sc itaanza na Bandari fc ya katika nusu fainali ya kwanza itakayopigwa saa nane mchana katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Bandari imefika hatua hiyo baada ya kuwatoa Singida united wakati Simba wao wamewafurusha Afc Leopard ya Kenya.

Haruna Niyonzima akimtoka mchezaji wa Afc Leopard.

Nusu fainali ya pili inawakutanisha wabishi wa Kenya dhidi ya wabishi wa Tanzania. Ni Mbao fc dhidi ya Kariobangi Sharks mchezo utakaopigwa saa kumi za jioni siku ya Ijumaa pia.

Kwa ratiba hiyo inaifanya vita ya kuwania fainali ya Sportpesa Supercup kuikitanisha Tanzania dhidi ya Kenya katika vita ya kuwania kucheza na Everton ya Uingereza.

Sambaza....