Sambaza....

Unapomtaja kijana huyu, unataja kinda la Kitanzania lenye uwezo mkubwa kwa kucheza soka. Na hasa linapokuja jambo la kufunga silaha yake kubwa ni usahihi wa matendo, shabaha na kasi, ikiwemo maamuzi.

Hapa ndipo walinzi wengi hushindwa kumkaba kama ambavyo imedhihirika kwenye mchezo wa fainali ya Azam Federation ambapo katika mchezo mgumu kwenye safu inayoaminika kuwa ngumu ya ulinzi aliingia kambani mara 3.

Si jambo jepesi kwa mchezo wa fainali mchezaji moja akafunga goli hizo kwa kuwa huwa tunaamini mechi hizo huwa na nafasi finyu sana ya kufunga.

Sopu kama ambayo anatambulika licha ya umri mdogo ni mchezaji aliyepita njia sahihi za makuzi ya kisoka ambayo yanampa uzoefu wa kufanya haya tunayoyaona sasa.

Alilelewa kwenye kikosi cha pili cha vijana lake Simba na baadaye kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya AFCON ya Vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 Gabon mwaka 2017.

Akiwa na wenzake kadha ambao pia walihusika na mchezo huo wa fainali mfano ni Dickson Job ,Kibwana Shomari kwa upande wa Yanga ,Rashid Chambo, Muhsin Makame naye Sopu ni zao la Bakaro Shime pamoja na Kim Poulsen.

Alianza ligi kuu akiwa na Ndanda na alikuwemo katika msimu ambayo iliporomoka daraja. Kwa kile alichokifanya kwenye mchezo huu kinatoa funzo kubwa juu ya uwekezaji kwenye soka la vijana.

Utajiuliza maswali mengi sana juu yake ‘Kwanini alikuwa mwiba sana kwa Yanga katika mchezo huu wa fainali?

Jibu langu la kiufundi litasimama katika maeneo tatu, uwezo mkubwa wa kusoma udhaifu wa wapinzani, kasi yake ,kujiamini kwake .

Mjumuiko wa vitu hivyo ulifanya kuwapa ‘ kalinyekalinye’ safu ya ulinzi wa Yanga iliyokuwa ikisifiwa tangu mwanzo wa msimu.

Kuwa ni ngumu kupitika na golikipa ndiyo kabisaa ‘hatari ya danger’ lakini si kwa Sopu aliifanya kuwa’ nyanya’.

Sub ya Mwamnyeto na Djuma Shabani inaweza ikakazia hili jumla walishindwa kumthibiti Sopu.

Kwa maana nyingine unweza kusema Coastal wameshindwa kupata ubingwa lakini Sopu binafsi amekuwa bingwa.

Siyo jambo jepesi mchezo wowote duniani wenye hadhi ya fainali mchezaji moja akafunga magoli 3 japo huwa inatokea tutakubaliana kuwa ni kwa nadra sana.

Sopu alivunjavunja ile ‘partnership ‘ ya Job na Mwamnyeto ya ndani ya klabu na timu ya Taifa, maana huwa wanacheza hivyo hivyo.

Yanga kama Yanga nao wanafaida na mechi hii kwenye maeneo kadhaa ukiachilia mbali ubingwa pia wametambua udhaifu mkubwa uliopo kwenye safu yao ya ulinzi kuelekea mashindano ya kimataifa .


Sambaza....