Sambaza....

Kuelekea mtanange wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly Cairo dhidi ya Al Hilal ya Sudan koch mkuu wa Ahly amesema wamejiandaa vyema kwenda kupata ushindi mbele ya Wasudan hao.

Marcell Koller kocha mkuu wa Al Ahly amesema uwepo wa mashabiki utawasaidia wachezaji wake kuweza kufikia lengo na kuvuka kwenda robo fainali.

 

“Ni lazima tushinde kwa goli moja au kwa tofauti ya magoli mawili, na tutapigana hadi dakika ya mwisho ili kupata ushindi.

Idadi kubwa ya mashabiki watakaohudhuria itakuwa msaada mzuri kwa wachezaji kufikia lengo lao na kupata nafasi ya kufuzu,” alisema Marcel Koller

Nae kocha Mcongo wa Al Hilal Florentine Ibenge amesema anafurahia kucheza mbele ya mashabiki elfu hamsini watakaohudhuria mchezo huo na wapo tayari kuwashangaza Ahly na kufuzu kwenda robo fainali.

Al Hilal waliibuka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa kwanza uliopigwa Sudan

Florentine Ibenge “Tuko hapa Cairo kufuzu kwa robo-fainali ya CAF Champions League na pia kuwafurahisha wafuasi wetu.”

“Ni habari njema kwetu kwamba kutakuwa na mashabiki 50,000 wa Al Ahly watakaoruhusiwa kuhudhuria mchezo huo na nina furaha kuishi katika mazingira kama haya licha ya kwamba wao si wafuasi wa timu yangu,” aliongeza Florentine Ibenge

Katika mchezo huo sare ya aina yoyote itamfanya Al Hilal kuungana na Mamelody kufuzu kutoka katika kundi lao, wakati kwa Al Ahly wanapaswa kupata ushindi ili kuvuka na kwenda robo fainali.

Sambaza....