Wapwa : Waswahili wanao msemo wao kufa kufaana …..
Baada ya kamati ya saa 72 kumfungia Bernard Morrison kucheza michezo mitatu ya ligi kuu ya NBC itakayofuata
Ambao ni dhidi ya Ruvu shooting ,Namungo na Simba sports baadaye mwezi October
Kuna maswali mengi nimekuwa naulizwa kubwa kuliko wengi wa akiuliza adhabu hii inaenda kimataifa au ni kwa ligi ya ndani tu
Lakini Mimi nikaibua swali jingine akilini Morrison ni mchezaji anayecheza kikosi cha kwanza kama hana tatizo lolote liwe la afya au la kikanuni
Tumeona Kocha Nabi akimuamini kuanza kiungo moja wapo wa pembeni hasa kule kushoto!
Swali hapa nani atakayenufaika kifungo cha siku 20 atakazokosekana Morrison
nani ataanza kwenye nafasi yake pale
Faridi ambaye mara nyingi Morrison akiwepo yeye anakuwa chaguo la pili au Moloko Nkane na Ambundo kwenye kuajust a just kutamfanya akakaimu jimbo
Kwa muda hadi atakavyorejea Mbunge Morrison? ni wakati ambao tunaweza kumuona mchezaji kama Makambo kuanza upande ule wa mguu wakushoto?
Ujue kupungua kwa Morrison kunaweza kutoa nafasi Kwa wachezaji wengi hata wa nje ya position hiyo ,hii itatokana na adjustments ambayo effect ni Morrison
Mfano Ngushi kama Makambo atachezeshwa kama kiungo wa kushoto yakatokea mahitaji ya ushambuliaji wa kati
Very possible kuingia huyu Kijana lakini pia kuna Tuisila Kisinda Mimi hupenda kumuita T-Better ( Moja ya pikipiki yenye kasi) kutokana na Play style yake
Hofu yangu ya ujumla kwa Morrison yeye binafsi ni pale ambapo kuna mchezaji kamshawishi ipasavyo Professor Nabi kwa mechi hizo tatu zijazo nafasi ya ‘ Wakili msomi’ itabaki vile vile au ndiyo hoja yangu ya mwanzo kufa kufaana…