Nahodha wa zamani wa Azam fc na wa sasa wa Simba Sports Club amefanikiwa kufunga magoli 100 katika Ligi Kuu Bara baada ya kuvitumikia vilabu viwili vikubwa nchini Tanzania yaani Simba Sc na Azam fc.
Katika magoli 100 ya Bocco aliyafunga kuanzia mwaka 2008 katika msimu wake wa kwanza akiwa na Azam mpaka kufikia mwaka huu akiwa na SimbaSc. Ambapo magoli 84 aliyafunga akiwa na Azam huku 16 akifunga akiwa na Simba.
Mchanganuo wa magoli Bocco!
Septemba 24, 2008, John Bocco alifungua akaunti yake ya mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania pale alipoisaidia Azam FC kushinda 2-0 dhidi ya Toto Africa ya Mwanza.
Bao lake la dakika ya 38 lilikuwa la pili katika mchezo huo, baada ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kufunga bao la kwanza mapema dakika ya 6.
Mabao 100 ya Ligi ya John Bocco yako katika mchanganuo ufuatao.
*Takwimu sahihi ni magoli tu
Miaka 10 baadaye, 2018, John Bocco alifikisha mabao 98 kwenye Ligi Kuu msimu jana. Akawa amebakiza mabao mawili kufikisha jumla ya idadi ya magoli 100.
Msimu wa mwaka 2017/2018 ndiyo tulishuhudia pia John Bocco akishinda tuzo yake ya kwanza ya mchezaji bora wa VPL, tuzo ambayo kimsingi alistahili kuipata miaka mingi iliyopita.
Msimu wake wa pili, 2009/10, John Bocco alifunga mabao 14 kwenye VPL na alitoa mchango mkubwa sana kwa Azam FC iliyomaliza Ligi kwenye nafasi ya tatu lakini kura hazikutosha kumpa uchezaji bora wa ligi kuu.
Mussa Hassan Mgosi – 18
John Bocco – 14
Mrisho Ngassa – 14
Msimu wa 2011/12, John Bocco alikuwa wa moto na alistahili kuwa mchezaji bora wa VPL, alifunga mabao 19 yaliyompatia tuzo ya kiatu cha dhahabu lakini akabaniwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.