Mshambuliaji Fiston Mayele amekua akifanya vyema akiwa na Yanga na hivyo kupeleka baadhi ya vilabu nchini Afrika Kusini kutajwa kuhitaji huduma yake. Miongoni mwa vilabu vinavyotajwa ni Kazier Chiefs na Mamelodi Sundows.
Akizungumzia uhitaji huo wa nyota wake Rais wa Yanga Hersi Said ameiambia FARPost “Hatujapokea mawasiliano rasmi kutoka kwa klabu yoyote ya PSL kuhusu Fiston Mayele,”
Lakini pia yeye mwenyewe Fiston Mayele amesema hajapokea ofa yoyote kutoka timu yoyote ile wala viongozi wake hawana ofa pia kumhusu yeye “Ninaona uvumi, lakini sijawahi kuzungumza na mtu yeyote kutoka klabu, wala uongozi wangu haujazungumza na mtu yeyote katika Chiefs,” Mayele aliiambia FARPPost
Nyota wa karibu na Fiston Mayele amesema mshambuliaji huyo amekua akiifwatili Ligi ya Afrika Kusini na kupelekea kuchochea uvumi wa kumuhusu nyota huyo kutimkia nchini humo “Anafuatilia PSL sana na anaona kuyumba kwa Chiefs. Ni wazi kwamba inamtia wasiwasi, na kama angepata nafasi ya kujiunga na timu nyingine isipokuwa Chiefs, angefanya hivyo. Kwa kweli sio juu ya timu ambazo angependa kujiunga nazo,” kilisema chanzo hicho.
Inasemekana Sundowns pia ilikua ikimfwatilia mchezaji huyo na kuandaa ripoti ya kina kuhusu yeye. Akiwa Rustenburg wiki iliyopita kabla ya mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo, aliripotiwa kutembelewa na mwakilishi wa Sundowns.
“Walimfikia, ingawa sio rasmi. Ilitoa picha ya kile angetarajia kutoka kwa Sundowns. Ikiwa kuna klabu ya Afrika Kusini ambayo angejiunga nayo kwa furaha, ni Sundowns,” mchezaji huyo alifichua.
Kulingana na yeye, Masandawana ni timu ambayo Mayele angetamani kujiunga nayo ikiwa watamfuata na kuhitaji huduma yake. Tayari Mamelodi ni mabingwa wa PSL hivyo watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.