Sambaza....

Mpaka sasa katika Ligi ya NBC imeshachezwa michezo ishirini na miwili kwa timu zote huku Yanga wakiwa kileleni mwa Ligi hiyo iliyobakisha michezo nane pekee kumalizika. Yanga yupo kileleni akifwatiwa na Simba walioachwa kwa tofauti ya alama sita.

Katika mzungu huo wa 22 wa Ligi tayari kuna wachezaji wanaoendelea kufanya vyema na kupelekea ushindani mkali katika takwimu Ligi ikielekea ukiongoni. Baadhi ya takwimu hizo ni pamoja na pasi za mabao, mfungaji bora na makipa waliotoka uwanjani bila nyavu zao kutikiswa “cleansheet”.

Katika takwimu hizo mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele wa Yanga ndie kinara wa mabao akiwa na mabao 15 mbele ya Saidoo Ntibazonkiza na Moses Phiri wote wa Simba wakiwa na mabao 10 huku wakifwatiwa na John Bocco (Simba) na Bruno Gomez (Singida) wenye mabao 9.

Katika kutengeneza mabao Clatous Chama wa Simba ndie kinara akiwa na pasi 14 za mabao “assist” halafu anafwatiwa na Saido Ntibazonkiza mwenye pasi 8 za mabao. Pia yupo Ayoub Lyanga mwenye pasi 7 na Sixtus Sabilo mwenye pasi 6 za mabao.

Kwa upande wa makipa ni Djigui Diara wa Yanga ndio kinara ambapo ana “cleansheet” 13 akiwaacha Manula wa Simba yeye ana 11 na Ali Ahmada wa Azam Fc mwenye “clean sheet” 8. Halafu wapo kina Metacha Mnata, Mohamed Mroivil na Said Kipao wote wakiwa na “clean sheet” 6.

Kwa ujumla ukitazama katika sehemu zote tatu utaona kila eneo angalua Simba ina mchezaji/wachezaji wanaofanya vyema. Katika ufungaji Saidoo na Phiri wamezidiwa na Mayele pekee lakini pia katika makipa Aishi Manula amezidiwa “clean sheet” mbili pekee na Diara wakati katika pasi za mabao wanaoongoza ni Saidoo na Chama katika kutoa pasi nyingi za mabao.

 

Kiungo wa Simba aliojiunga nao katika dirisha dogo akitokea Geita Gold ndio mchezaji aliehusika katika mabao mengi zaidi [mabao 20]. Saidoo ana mabao 10 na pia ana pasi za mabao 10 hivyo kumfanya kuwa kinara katika klabu yake ya Simba na Ligi nzima kwa ujumla.

Sambaza....