Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) siku ya Jumapili wametangaza namna makundi ya michuano ya Mataifa Afrika itakavyopangwa kwa kutoa mchangunuo wa makundi ya awali kabla ya kupangwa kwa makundi yenyewe April 12 mwaka huu mjini Cairo, Misri.
Katika mchanganuo huo Tanzania ambayo hii ni mara yake ya pili kufuzu kwenye mashindano hayo wamewekwa kwenye kundi la mwisho kabisa pamoja na nchini nyingine ya Afrika Mashariki Kenya.
Nchi nyingine ambazo ndio mara yao ya kwanza kufuzu kwenye michuano hii yaani Madagascar na Mauritania wao wamepangwa sehemu moja na Tanzania wakati Burundi wao wapo kwenye kundi namba tatu.
Droo itafanyika Ijumaa ya tarehe 12 mwezi huu sehemu ya kihistoria ya Giza Pyramids and Sphinx.
Katika makundi hayo inamaana kuwa kuna uwezekano mkubwa wa walio katika kundi la kwanza kutopangwa kwenye kundi moja la Michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Michuano hii itafanyika Misri baada ya Cameroon kupokonywa nafasi ya kuandaa kutokana na kutokuwa na kusuasua kwa maandalizi ambapo kwa mara ya kwanza itajumuisha imu 24 wanachama wa CAF.