Sambaza....

Jana Barcelona wamefanikiwa kukamilisha vipimo vya Phillipe Countinho.

Hivo rasmi ni mchezaji wa Barcelona , anachosubiri ni kukabidhiwa namba ya jezi atakayoivaa.

Yuko kwenye ardhi ambayo alitabiriwa na wengi kama gwiji wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho Gaucho.

Ronaldinho aliwahi kusema mtu pekee anayeweza kuziba pengo la Neymar ni Phillipe Countinho.

Muda huu tayari Phillipe Countinho yupo sehemu ambayo alikuwa anaitamani na wengi waliona ni sehemu sahihi ambayo itamfaa kucheza.

Ameshakuwa mchezaji wa Barcelona tayari. Je ataenda kucheza katika mfumo ambao utamfaa ??

Barcelona msimuu huu wamecheza mifumo kadhaa kama 4-4-2, 4-3-3, 4-2-3-1.

Ndani ya mifumo hii Countinho atafanikiwa kuchezaje ?

4-3-3. Huu ni mfumo ambao unakuwa na mabeki wanne, viungo watatu wa kati na washambuliaji watatu ambapo wawili watakuwa wanatokea pembeni na mmoja kusimama kama mshambuliaji wa kati.

Katika mfumo huu Countinho anaweza kusimama kama mtu wa kuziba pengo la Neymar. Kwa sababu anaweza akawa anacheza kama mshambuliaji anayetokea pembeni kushoto kama ambavyo alivyokuwa anacheza Neymar.

Katika mfumo huu Phillipe Countinho kule mbele anauwezo wa kucheza pamoja na Messi ambaye atacheza kama mshambuliaji wa pembeni akitokea kulia, na Suarez atacheza kama mshambuliaji wa kati.

Kwenye huu mfumo pia, Countinho anaweza kutumika kama mtu wa kuziba nafasi ya Iniesta.

Iniesta kwa sasa umri unakwenda, Phillipe Countinho anaonekana kama ni mtu ambaye amekuja kwa ajili ya kumpumzisha Iniesta.

Hivo Phillipe Countinho anaweza akawa anacheza kwa kutokea katikati mwa uwanja.

Hivo kule mbele kuwapa nafasi Dembele, Suarez na Messi kucheza huku yeye akicheza katikati akicheza na Sergio/Rakitic, Paulinho na yeye mwenyewe.

Katika mfumo wa 4-4-2, iwe Flat au Diamond anaweza akacheza vizuri akitokea pembeni kushoto.

4-2-3-1 hapa anaweza akacheza kwa kutokea katikati kushoto , mfumo huu unaruhusu viungo wawili wa kati ambapo kwenye viungo hao wa kati anaweza akacheza Sergio Bosquets na Iniesta huku kwa wachezaji watatu watakaocheza mbele yao wanaweza kucheza Countinho ambaye atatokea pembeni kushoto, Messi ambaye atatokea katikati na Dembele ambaye atacheza pembeni kulia huku mshambuliaji wa mwisho akabaki kuwa Suarez.

Baada ya kuangalia jinsi ambavyo Countinho anaweza kucheza vizuri katika mfumo wa Barcelona, hebu tuangalie ubora wa Phillipe Countinho uko wapi ?

Uwezo wa kuona na kujitengenezea uwazi ndani ya uwanja.

Moja ya sifa ya Phillipe Countinho ni kukimbia na mpira, anapokuwa anakimbia na mpira huwa anatoa pasi kwa wenzake na kujiweka sehemu ambayo ina uwazi ili apokee tena mpira.

Uwezo huu wa kujitengenezea uwazi , huwa unampa nafasi ya kuonesha madhara akiwa karibu na goli kwa sababu wakati anapotoa pasi na kwenda sehemu ambayo ni wazi huwa anauwezo mkubwa wa kupiga mashuti ambayo yana madhara.

Ubora mwingine wa Phillipe Countinho ni uwezo wake wa kutengeneza muunganiko wa mashambulizi ndani ya timu.

Phillipe Countinho akiwa anacheza katikati ya uwanja, hushuka chini kuchukua mpira na kuanzisha mashambulizi. Mpaka sasa Phillipe Countinho ana take ons 39 ambazo ni nyingi kuzidi take ons za Iniesta na Paulinho. Mchezaji pekee wa Barcelona anayemzidi Take ons ni Messi.

Pia, Phillipe Countinho ni mzuri katika ufungaji na kutoa pasi za mwisho za magoli.

Barcelona haina tatizo la magoli lakini ujio wake utakuwa umeongeza uzito katika magoli na upatikanaji wa magoli ( utengenezwaji wa magoli).

Barcelona ina Messi ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza mipira iliyokufa ( mipira ya adhabu ndogo au free kick).

Phillipe Countinho ni mzuri sana eneo hili pia. Hivo anaingia kwenye kikosi cha Barcelona kuongeza nguvu kwenye eneo hili.

Hivo, Ujio wa Phillipe Countinho umeonesha namna sahihi ambavyo Barcelona walivyotakiwa kutumia pesa za Neymar kwa busara.

Sambaza....