Katika makala ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup kati ya Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa “Kwa Mkapa” tumekuwekea wachezaji 18 ambao huenda wakaanza katika mchezo huo.
Kama kawaida Simba inategemewa kuaingia katika mchezo huo wakiwa na lengo la kushambulia tu huku wakiendelea kutumia mbinu zao zile zile za viungo wengi na mpira wa kuvutia. Imekua ni kawaida kwa Simba kuendelea na mbinu zao za kucheza soka safi na kushambulia bila kujali inacheza na mpinzani wa aina gani.
Lakini upande wa pili mara nyingi wapinzani wa Simba ndio huwa na mikakati maalumu ya jinsi ya kucheza na Simba na hii ni kutokana na ubora wa klabu ya Simba.
Yanga wao wanaingia uwanjani kesho kibabe wakitoka kupata alama nne mbele ya Simba msimu huu, lakini pia wanakwenda kama timu yenye kutaka matokeo ya ushindi tu na si vinginevyo.
Ili kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao ni lazima wanyakue kombe la FA, ili kubeba kombe la FA ni lazima kuifunga Simba nusu fainali. Yanga katika mchezo wa kesho watakua na machaguo matatu ambayo ni Ushindi, Ushindi, Ushindi.
Kikosi cha Simba
Baada kocha Sven kuambulia sare na kipigo mbele ya Yanga katika michezo miwili ya msimu huu ni wazi mchezo wa kesho utakua wa muhimu kwake kuweza kulipiza kisasi na pia kudhihirisha ubora wake. Kuzifunga Ndanda, Lipuli ama Coastal bado hakukufanyi kuoenekana kua bora kama utashindwa kumfunga mpinzani mkubwa ambae ni Yanga.
Katika mchezo wa mwisho wa Ligi dhidi ya Namungo alipumzisha nyota wake wengi huku walitegemewa kuanza mchezo dhdi ya Yanga. Chama, Miquissone, Mkude, Bocco, Nyoni, Manula wote hawa walikua jukwaani kabisa. Ji wazi kabisa Sven mipango yake ya ushindi imeegemea kwa nyota hao.
Huende kikosi kikawa hivi:
1. Manula
2. Haruna Shamte
3. Mohamed Hussein
4. Pascal Wawa
5. Erasto Nyoni
6. Jonas Mkude
7. Luis Miquissone
8. Fraga Vieira
9.John Bocco
10. Clatous Chama
11. Deo Kanda.
Sub: Kakolanya, Gadiel, Kennedy, Ndemla, Dilunga, Kahata na Kagere!
Kikosi cha Yanga!
Mwalim Luc pamoja na msaidizi wake Master Mkwassa ni wazi wana mchezo mmoja pekee wa kesho ili kuamua hatma ya Yanga katika msimu ujao baada ya kukosa ubingwa wa Ligi sasa wamebaki na kombe la FA.
Yanga inakwenda kukutana na Simba ikiwa na changamoto ya majeruhi haswa ya wachezaji wake muhimu kabisa. Papy, Balama na Haruna Niyonzima wataukosa mchezo huo huku wachezaji wote hao wakiwa ni wa eneo muhimu la kiungo.
Katika michezo yote miwili yamwanzo ya msimu huu watatu hao walikua sehemu muhimu ya mbinu za Yanga eneo la katikati na kuweza kupata alama nne. Ni wazi sasa Luc atakwenda kuwatumia Yondani, Makame, Feisal au Ngassa katika eneo la kiungo.
Kikosi cha Yanga kitakua hivi:
1. Menata
2. Deus Kaseke
3. Japhary Mohamed
4. Said Makapu
5. Lamine Moro
6. Kelvin Yondani
7. Ditram Nchimbi
8. Abdulaziz Makame
9. David Molinga
10. Feisal Salum
11. Benard Morisson.
Sub: Shikalo, Dante, Ally Sonso, Raphael Daud, Sibomana, Ngassa, Tariq Seif.
Yote kwa yote jibu la mtanange huu tutalipa baada ya dakika 90 ambapo kama watatoka sare zitaongezwa dakika 30 na mpaka mikwaju ya matuta endapa mshindi hatopatikana katika dakika 120.
Nani kuibuka mbabe katika mchezo huu wa tatu msimu huu, Simba au Yanga? Kwangu mimi naiona sare katika dakika 90 mzigo utanalizwa katika dakika za nyongeza ama matuta kabisa.