Historia imeandika na rekodi imewekwa katika Dimba la Benjamin Mkapa na Yanga baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.
Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya US Monastir na kufikisha alama 10 katika kundi lake na kupelekea kufuzu kwenda hatua ya robo fainali wao na US Monastir na kuwaacha TP Mazembe pamoja na Real Bamako katika kundi D.
Yanga walioutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa licha ya mvua kuufanya uwanja kuwa na utelezi walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 33 kupitia kwa Kenedy Musonda aliyeunganisha krosi ya Jesus Moloko na kuwapeleka Yanga mapumziko wakiwa mbele.
Fiston Kalala Mayele alihitimisha ushindi wa Yanga katika dakika ya 59 baada ya kupokea pasi safi na kupiga shuti la chinichini lililomshinda mlinda mlango wa Monastir.
Yanga si tu walipata ushindi lakini pia walicheza vyema katika dakika zote 90 na kuwadhibiti kabisa Monastir ambao hawakupata hata nafasi yakupiga shuti lililolenga lango.
Kwa ushindi huo sasa unaipeleka Yanga robo fainali baada yakushindwa kufanya hivyo mwaka 2016 na 2018 walipoingia hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Shirikisho Afrika
Kikosi cha Yanga kilichoanza.
1. Djigui Diara
2. Djuma Shaban
3. Lomalisa Mutambala
4. Ibrahim Bacca
5. Bakari Nondo
6. Khalid Aucho
7. Jesus Moloko
8. Yanick Bangala
9. Fiston Mayele
10. Salum Aboubacar
11. Kenedy Musonda
Sub: Metacha, Job, Kibwana, Aziz Ki, Mudathir, Farid, Kisinda, Mzize
Kikosi cha US Monastir
1. Sadock Yedes
2. Saleh Harabi
3. Ousmane Adama
4. Houssem TKA
5. Dridi Ala
6. Ameur Omrani
7. Abdekhakim Amokrane
8. Zied Aloui
9. Hichem Baccer
10. Abdelkader Boutiche
11. Mohamed Saghaoui
Sub: Besbes, Khefacha, Dally, Jafeli, Traore, Othmen, Charefedine.