Sambaza....

Azam Fc itamkaribisha kwa mara ya kwanza Yanga katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex

Rekodi za mashindano yote kati ya hizi timu.

Timu hizi zimekutana mara 31 kwenye mashindano yote. Yanga imeshinda mara 12, Azam FC imeshinda mara 11 na zimetoka sare mara 8. Yanga imefunga mabao 41 na Azam FC imefunga mabao 40.

Hiki hapa ni kikosi changu cha pamoja kati ya Azam Fc na Yanga.

Kikosi hiki kitatumia mfumo wa 3-5-2.

Golikipa atakuwa Razak Abalora. Hapana shaka huyu ndiye golikipa bora wa msimu huu mpaka sasa ndiye golikipa aliyefungwa goli chache kwenye ligi kuu na akiwa na clean sheets nyingi.

Mabeki watatu wa kati.

Central Back Right, Agrey Moris. Amefanikiwa kutengeneza ukuta imara kati yake na Yakubu Mohammed. Kwenye kikosi hiki cha pamoja atacheza kama beki wa kati kulia.

Central Back, Yakubu Mohammed. Utulivu wake, uongozi wake katika timu na uimara katika kuokoa hatari unampa nafasi ya kuingia katika kikosi hiki bora cha pamoja akicheza kama beki wa kati.

Central Back Left, Kelvin Yondan. Amekuwa na msimu mzuri sana, kipindi ambacho anakosekana Yanga huyumba eneo la nyuma. Ni kiongozi mwingine katika eneo hili la nyuma na anafanikiwa kuingia kwenye kikosi cha pamoja kama beki wa kati kulia.

Wingback right: Hassan Kessy, alikuwa benchi muda mrefu lakini kuanzia mechi ya Mbao akaanza kupata nafasi taratibu, kombe la mapinduzi limemrudisha kwenye kiwango chake, uwezo wake wa kupanda na kushuka hivo hii inampa nafasi ya kucheza kama Wingback upande wa kulia.

Image result for yanga vs azam

Wingback left, Bruce Kangwa. Moja ya sifa kubwa ya Wingback ni kuleta uwiano mzuri kati ya kushambulia na kuzuia. Bruce Kangwa anauwezo mzuri wa kuleta uwiano katika maeneo haya mawili.

Viungo wa kati.

Stephano Kingue, ni kiungo bora katika eneo la ukabaji, na kwenye kikosi hiki atacheza kama kiungo wa kuzuia akiwalinda mabeki watatu.

Papy Kabamba. Anaweza kucheza pia kama kiungo wa kuzuia. Lakini kwenye kikosi hiki hatocheza eneo la kuzuia, ila atacheza kama box to box middfierder. Atakuwa na uwezo wa kupanda kushambulia kwa sababu anauwezo wa kukimbia kila eneo ambalo mpira ƴupo, pia anauwezo wa kushuka chini kusaidia kukaba.

Salum Abubakar. Stephano Kingue na Papy watakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia au kujilinda hii itampa uhuru Salum Abubakar kuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji.

Washambuliaji ni wawili.

Ibrahim Ajib na Yahya Zayd kwenye kikosi hiki atacheza kama mshambuliaji wa pili nyuma ya Yahya Zayd

Sambaza....