Sambaza....

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Adel Amrouche ametaja kikosi kitakachovaana na Niger katika mchezo wa kufuzu Afcon nchini Cameroon.

Stars yenye alama nne sawa na Uganda wakiwa nyuma ya Algeria vinara wanahitaji ushindi leo ili kuweka hai matumaini yao yakufuzu michuano hiyo ya Afcon kwa mara ya tatu.

Kikosi kamili cha Stars ni  walinda mlango Metacha Mnata (Yanga) Benno Kakolanya (Simba), Makame Vuai (KMKM) na Zuberi Foba (Azam).

Adel Ameouche, Kocha wa Taifa Stars.

Walinzi ni Datius Peter (Kagera Sugar), Dickson Job, Kibwana Shomary, Bakari Nondo Mwamnyeto na  Ibrahim Bacca (Yanga), Mohamed Hussein Zimbwe Jr, Kennedy Juma (Simba), Novatus Dismac (Zulte, Ubelgiji) Abdi Banda (Chippa, South Africa) na Lameck Lawi (Costal Union).

Kwenye eneo la kiungo kuna Himid Mao Mkami (Ghazl, Egypt), Adolph Mtasingwa Bitegeko (Völsungur ÍF, Iceland), Aziz Andambwile (Singida), Muzamir Yassin (Simba), Mudathir Yahya (Yanga), Ayoub Idrissa Bilal (Ankara, Uturuki), Ben Starkie (Basford Utd, England), Morris Abraham (Spartak Subotica, Serbia).

Na washambuliaji ni pamoja na  Simon Msuva (Al Qadsiah, Saudi), Abdul Suleiman Sopu (Azam), Kibu Dennis Prosper (Simba)
John Tiber (Hatta Club UAE), Bernard Kamungo (FC Dallas, USA), Adi Yusuph (Brackley Town, England) na 
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).

Kikosi cha Stars kikiwa mazoezini kujiandaa na michezo ya kufuzu Afcon

Msemaji wa TFF Cliford Marion Ndimbo tayari ametaja viingilio vya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa kumi jioni siku ya Jumapili.

“Katika mchezo huo muhimu wa nchi viingio vitakua ni 3000 kwa mzunguko na 10,000 kwa VIP B&C, wakati VIP A hazitauzwa zitatolewa kwa mualiko maalum,” alisema Ndimbo.

Sambaza....