Sambaza....

Mabingwa wa Kihistoria wa kombe la Ligi Kuu Bara Yanga sc  ni kama wameshituka na kuamua kurudi katika njia za kibingwa baada ya kusota kwa miaka mitatu mfululizo bila kikombe chochote cha Ligi Kuu.

Iko hivi baada ya aliekua mdhamini wao Yusuph Manji kuondoka klabuni hapo uchumi wa klabu ukaanza kuyumba na kua dhohofu na kupelekea kushindwa kutoa upinzani wakweli kwa Watani zao Simba.

Simba chini ya Mwenyenyiki wa Bodi Mohamed Dewji wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 3 mfululizo huku wakiendelea kujinasibu kuuchukua ubingwa huo mara 10 mfululizo.

Nahodha wa Simba John Bocco akikabidhiwa kombe na ubingwa wa VPL na Mheshimiwa Hamis Kigwangara.

“Tutachukua kombe la Ligi Kuu back to back mara 10” Hajji Manara, ni moja ya kauli anayopenda kutamba nayo msemaji wa klabu ya Simba

Usifikiri hii kauli watu wa Yanga hawaisikii na hawaifanyii kazi, hapana wapo wanajipanga kukata ngebe za Haji pamoja na klabu ya Simba kwa ujumla. Yanga wameona nyodo za Simba na mbwembwe zao zimetosha sasa kwa hii miaka mitatu na sasa ni wakati wao wa kurudisha enzi zao.

Yanga kupitia wadhamini wao GSM wamefanya usajili wa nguvu na kuondoa wachezaji wengi waliokua Yanga msimu uliomalizika ambao kwa kiasi kikubwa waliifelisha Yanga kutokana na viwango vyao vidogo.

Mrisho Ngassa “Uncle”

Molinga, Yikpe, Ngassa, Japhary, Tshishimbi, Dante, Sibomana ni miongoni wa majina yaliyokutana na panga la Yanga wakitakiwa kupisha nafasi kwa nyota wapya wa Yanga na kuisuka Yanga mpya.

GSM walishabeba dhamana ya kuisuka Yanga mpya huku wakikiri msimu ujao wanakwenda kurejesha furaha na makombe katika mitaa ya Twiga na Jangwani.

“Msimu ujao Yanga ikikosa ubingwa tuulizwe sisi GSM” Mhandisi Hesri Said alisisitiza katika moja ya kauli zake kwa Wanayanga kuelekea msimu ujao.

Kwa usajili wa Yanga kwa msimu huu maana yake wameamua kusogea mstari wa mbele katika vita ya kuwania ubingwa na si kujipanga kwaajili ya baadae. Yanga wamesajili wachezaji wa nje na ndani ya nchi ambao wapo tayari kwa mapambano na si kusubiri wapate ukomavu.

Waziri Junior, Bakari Mwamunyeto, Abdalah Shaibu, Yassin Mustapha ni nyota wakomavu na waliofanya vizuri msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara ambao wanakwenda kuungana na nyota wa kigeni kama Carlinho’s, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong na Yakoube Sogne.

Waziri Junior

Bila kusahau Yanga imewabakisha nyota muhimu wa msimu uliomalizika kina Feisal, Kaseke, Metacha, Nchimbi na Niyonzima ambao watakwenda kuungana na wachezaji wapya kuunda Yanga ya ubingwa.

Hakika kwa usajili huu Yanga wameamua kwenda kuwa washindani wa ubingwa dhidi ya Simba bila kuwasahau Azam fc.

Tazama kikosi kamili cha Yanga litakavyokua kua msimu ujao utaona jinsi kilivyosheheni katika kila idara kukiwa na wachezaji wenye uwezo unaokaribiana.

Bakari Mwamunyeto na Abdalah Shaibu “Ninja”

Walinda Mlango:
Farouk Shikalo 🇰🇪
Metacha Mnata 🇹🇿
Ramadhan Kabwili 🇹🇿

Walinzi wa katikati
Lamine Moro 🇬🇭
Said Juma Makapu 🇹🇿
Abdallah Shaibu Ninja 🇹🇿
Bakari Nondo Mwamnyeto🇹🇿

Walinzi wa pembeni
Paul Godfrey “Boxer” 🇹🇿
Kibwana Shomari 🇹🇿                                          Yasin Mustapha 🇹🇿
Adeyoun Saleh 🇹🇿

Viungo wa katikati:
Feisal Salum Abdallah “Fei Toto” 🇹🇿
Haruna Akizimana Niyonzima 🇷🇼
Abdulaziz Makame “Bui” 🇹🇿
Zawadi “Gift” Mauya 🇹🇿
Mukoko Tonombe 🇨🇩                                 Carlinhos 🇦🇴

Carlinho

Viungo wa pembeni
Balama Mapinduzi “Kipenseli” 🇹🇿
Deus Kaseke 🇹🇿
Juma Mahadhi 🇹🇿
Tuinsila Kisinda 🇨🇩
Farid Mussa 🇹🇿

Washambuliaji
Michael Sarpong 🇬🇭
Waziri Junior 🇹🇿
Ditram Nchimbi “Duma” 🇹🇿
Yocouba Songne 🇧🇫

Sambaza....