Sambaza....

Kesho Kariakoo derby itapigwa kunako uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam, mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba SC, dhidi ya Yanga SC

Hakika utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwa kutazamia ubora wa vikosi, uhitaji wa alama tatu na nafasi katika jedwari la ligi hiyo

Simba SC, ndio vinara wa ligi hiyo hadi sasa wakiwa na alama 58, baada ya kushuka dimbani mara 23, ni wazi wataingia katika mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha wanakusanya alama tatu ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa, pia kutunza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa ligi hiyo hadi sasa

KIUFUNDI

Simba SC, wanaotumia sana mfumo wa 3-5-2 ni wazuri sana kwenye kumiliki mpira, pressing na cut of ni wazi unapouzungumzia ubora wa kikosi chao kwa sasa utaanzia kunako eneo lake la kiungo, safu hii ndio imekuwa mhimili wa timu katika kuamua mchezo

Uwepo wa utajiri mkubwa wa viungo wenye skills nzuri, umeifanya safu hii kuwa imara sana watu kama Jonas Mkude, James Kotei, Mzamir Yasin, Said Ndemla, Shiza Kichuya n,k wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuhakikisha timu inakuwa na umiliki mzuri wa mpira

Pia safu yake ya ulinzi imekuwa ikicheza kwa uelewano mkubwa, na kujenga uimara kwa kiasi fulani japo kuna wakati hufanya makosa binafsi yanayozaa mabao, lakini ni wazuri kwa kufanya basic buildup ili kujenda flow ya timu yao hapa ndipo kwenye ubora mwingine wa Simba SC

Tactical Philosophy

Simba wamekuwa wakihakikisha wanacheza katika falsafa yao kwa muda wote wa mchezo, sio timu nyepesi kuivuruga katika aina yao ya uchezaji hivyo Yanga watatakiwa kufanya kazi ya ziada endapo watafikilia kushindana na Simba katika hili

Tactical deployment ya 3-5-2 hii imeonekana kinufaisha sana Simba SC, kutokana na kuongeza wigo wa kutumia wachezaji wengi wenye uwezo wa kuchezo soka la kushambulia huku pressing game ikisimama kama mtaji wao mkubwa

Kuua full back roles, imeifanya Simba kuwa na uhakika wa mashmbulizi yake ya pande zote na pia kujilinda kwa maana na mabeki wake kuingia ndani kama viungo wakabaji wa ziada hali inayoongeza uimara kwenye defensive patterns zao, hii itailadhimu Yanga kufanya mashambulizi yao kwa haraka sana ili kuweza kupata bao

Mfumo huo, umemfanya Shiza Kichuya kucheza kama creative midfielder akifanya technical dribbling ili kuiyumbisha back line iliyo kwenye mstari lakini pia akitakiwa kufanya switching to unlock na Emmanuel Okwi, hii imekuwa ikiwasaidia sana katika mashambulizi yao hali itakayowafanya viungo wa kati wa Yanga kucheza jirani na safu yao ulinzi ili kuua muunganiko huu

Bado naiona Simba ni hatari sana kuelekea katika mchezo huo, kwa counter attacking run, long ball game, finishing a speed ya Okwi, game technical understanding, changing style of play, tactical philosophy ya Pierre Rechantre na wana confidence sana kutokana na kupata matokeo mazuri katika michezo yao mingi

 

Emmanuel Okwi na John Bocco hawa ni wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao hadi sasa, hivyo mentality yao inaweza kuwa sumu katika mchezo huo

KWA UPANDE WA YANGA SC

Yanga SC, wao ndio mabingwa watetezi na wanashika nafasi ya pili kunako jedwali la ligi hiyo, wakiwa na alama 49, baada kushuka dimbani mara 23, hivyo huitaji wa alama tatu kwao una umuhimu mkubwa sana ili kufufua matuamini yao ya kutetea taji hilo

KIMBINU

Yanga wamekuwa wakicheza kwa mifumo tofauti kulingana na mpinzani wanayekutana naye alivyo, 4-4-2, 4-3-3 na 4-2-3-1 hii ni mifumo wanayoipendelea lakini katika mchezo wa kesho ni wazi wataanza na 4-2-3-1 (Unconventional formation) wakijaribu kuua muunganiko wa Simba katikati ya kiwanja

Huo unaweza kuwa mfumo utakaowasaidia sana katika mchezo huo, hii ni flexible formation ni rahisi kurudi katika mfumo mwingine lakini husaidia sana kuvunja muunganiko wa kimbinu mpinzani wa mpinzani katikati ya kiwanja

Yanga sio wazuri sana kwenye kumiliki mpira, lakini ni hatari sana katika aina yao ya uchezaji mara husukuma mipira kwenye advanced position kutokana na kuwa na dedicated strikers Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib hii huwasaidia sana katika kufanya attempts zao

Safu yake ya kiungo imeonekana kukosa ujazo wa kutosha, na mara nyingi wamekuwa wakimtegemea sana Papy Tshishimbi katika patterns zao huyu ucheza kama kiungo wa ulinzi pale timu inakosa mpira pia kucheza kama kiungo mchezeshaji pale timu inapokuwa na mpira (box to box midfielder) pengine urejeo wa Thaban Kamusoko unaweza kuongeza kitu katika mchezo huo

Watu kama Raphael Daud, Said Juma na Pius Buswita wamekuwa na impact kubwa kwenye eneo la kiungo hali itakayowaladhimu viungo wa Simba kufanya kazi ya ziada katikati ya kiwanja

Tactical philosophy

Yanga hucheza direct play, wamekuwa wazuri sana kwenye matumizi ya nguvu na long ball game, huku counter attacking play ikiwa ndio siraha yao kubwa hivyo safu ya ulinzi ya Simba watatakiwa kujipanga vema kwa aina hii ya mbinu

Mara nyingi hutumia sana flanks, katika kujilinda na kushambulia hii imewafanya Yanga kufunga mabao yao mengi kutokea pembeni hivyo Simba wanatakiwa kuwa makini sana pembeni mwa uwanja kuhakikisha wanakuwa maelewano mazuri sana wakati wa kujilinda

Bila shaka Yanga wataingia katika mchezo huu kama underdog, kutokana na ubora wa kikosi chao na aina yao ya uchezaji kwa sasa haitakuwa rahisi kwao kushindana na Simba katika umiliki wa mpira

Na vema Yanga wakafanya half way offensive ili kukataa kucheza mchezo wa kujilinda moja kwa moja kwa moja

Pia naiona Yanga inaweza kuwa hatari kwa Simba kutokana na mbinu zao, kwa namna wanavyoweza kutumia flanks, break through ama counter attacking play kupata mabao, pia wana confidence inayoweza kuwasaidia katika mchezo wa kesho

Obrey Chirwa ndiye kinara wa ufungaji mabao kunako kikosi cha Yanga, japo amekosa muendelezo mzuri katika kufunga lakini anapaswa kuchungwa sana pia mabao Yanga yamekuwa yakifungwa na wachezaji tofauti sana hii Simba wanapaswa kuwa na tahadhari nayo

Hii derby, na mara nyingi michezo ya namna hii utegemea game plans ama approach ya walimu vile wanavyoweza kushinda saikolojia za wachezaji wao kuelekea katika huu, hivyo sio aina ya mchezo ambao unawezea kutoa possibility kubwa ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi

Na kwa movements za timu zote naona kuna mabao watafungana hawa bila shaka

Sambaza....