Sambaza....

Kila mtu afanyapo vizuri anatamani kushikwa mkono na kuambiwa ‘kazi nzuri umefanya’, kushikwa mkono na mtu kutambua ulichofanya ni kizuri ni jambo ambalo hata mzazi anatakiwa kufanya kwa mwanae.

Ligi yetu ni kubwa sana, inachangamoto zake za ndani na nje ya uwanja, wachezaji na makocha wanaohusika wanapambana nazo hizi kila siku kabla, wakati na baada ya mchezo, sisi kama wadau ni jukumu letu kuwapa motisha kwa kile kizuri wafanyacho. Hivyo basi, tovuti ya kandanda.co.tz ikaja na kitu kinaitwa Galacha wa Mabao wa Kandanda kwa Mwezi.

Hii ni nini?
Tovuti kila baada ya mechi za ligi kuu Tanzania bara hurekodi matokeo ya mechi na wafungaji wake. Takwimu hizi zinahifadhiwa katika tovuti ya kandanda na zipo wazi kwa yeyote kuangalia. Takwimu hizi zinapangwa kwa msimu (jumla) na kwa mwezi. Kila mwezi tuangaalia nani amefunga magoli mengi zaidi, na huyo ndio anakuwa Galacha wa Mabao wa Kandanda kwa mwezi.

Lengo?
Lengo letu kuu ni kuthamini matunda ya wachezaji wetu na kuwapa motisha kwa hiki kidogo ambacho tunatoa kwaajili ya kusheherekea nao.

Mfungaji Bora mwezi wa Tisa wa ligi Kuu Tanzania bara, Eliud Ambokile, akiwa na zawadi yake kutoka katika tovuti ya kandanda ya kumpongeza.

Nani amepata mpaka sasa?
Kuanzia Agosti 3018 hadi Disemba 2018, hawa ndio wachezaji ambao Tovuti imesheherekea nao, Meddie Kagere (Simba Sc), Eliud Ambokile (Mbeya City Fc), Emmanuel Okwi (Simba) na Heritier Makambo (novemba na disemba) kutoka Yanga Sc kwa miezi miwili mfululizo.

Sambaza....