Klabu ya Simba kwa sasa ndie mwakilishi pekee wa nchi katika michuano ya Kimataifa baada ya kufuzu katika hatua ya makundi katika klabu bingwa Africa. Simba sc ipo kundi D pamoja na timu vigogo barani Africa kama Al-ahly na As Vita.
Klabu ya Simba tayari imejiwekea malengo ya kufuzu robo fainali huku wakiwa na kauli mbiu yao ya “YES WE CAN”. Wakiwa na maaana wako tayari kwa kupambana ili waweze kufika hatua ya robo fainali.
Simba sc tayari imeshacheza mchezo mmoja na kupata alama tatu katika uwanja wa nyumbani baada ya kuifunga JS Souara ya Algeria mabao matatu kwa sifuri. Huo ni mwanzo mzuri kwa timu yenye nia ya kuendelea mbele, kwa ushindi wa mchezo wa kwanza maana yake unawapa nguvu na kujiamini kuelekea michezo ijayo.
Hesabu za kuipeleka Simba robo faiali
Alama tisa nyumbani.
Simba sc wanatakiwa kutokupoteza hata alama moja katika uwanja wa nyumbani. Simba sc inatakiwa kushinda michezo yote mitatu tena kwa magoli pasipo kutoka sare wala kupoteza mchezo. Kwa ushindi dhidi ya JS Souara maana yake tayari wana alama tatu wakibakiwa kukusanya alama sita katikwa uwanja wa Taifa.
Sare ugenini
Ili kujiimarisha na kukusanya alama nyingi katika kundi lake ni vyema basi wakawa na hesabu za kupata angalau alama moja katika michezo migumu ya ugenini haswa dhidi ya Al-Ahly na AS Vita kuliko kupoteza kabisa alama zote tatu.
Kupoteza kwa magoli machache.
Simba inaenda kwenye michezo miwili migumu mfululizo, ambapo watakua ugenini dhidi katika nchi za Congo na Misri kwenda kupambana na wababe wa kundi AS Vita na Al-Ahly. Michezo hii miwili ni vyema basi Simba ikajiandaa vizuri kisaikolojia, hata kama watakubali kupoteza mchezo basi wasifungwe kwa idadi kubwa ya mabao ili isiwaribie kwenye utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa “Goal Difference”.
Alama Sita za JS Souara
Simba inatakiwa kuvuna alama zote sita kutoka kwa Js Souara ili kuweza kufidia endapo watapoteza dhidi ya Vita Club na Al-Ahly . Simba inatakiwa kuonyesha umwamba wake kwa klabu hii ndogo kutoka Algeria kutokana na Simba kuizidi historia katila michuano hii na hata ukubwa wa klabu.
Tofauti ya mabao
Simba inatakiwa kutumia vizuri nafasi wanazopata na kufunga magoli mengi ambayo huenda yakawasaidia mbeleni endapo watakua wamefungana alama. Katika mchezo wa juzi nilisikitishwa na wachezaji wa Simba jinsi walivyoridhika baada ya kupata ushindi dhidi ya Waalgeria. Kama mpinzani ameingia katika mfumo unamfunga tuu hata saba kama inawezekana.