
Klabu ya Simba leo imetaja jumla ya wachezaji 18 watakaokwenda Lubumbashi kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Africa.
Walinda mlango: Aishi Manula, Deo Dida
Walinzi: Zana Coulibaly, Asante Kwasi, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Paul Bukaba na Juuko Mursheed.
Viungo: Haruna Niyonzima, Mdhamiru Yasin, Said Ndemla, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga na Cleotus Chama.
Washambuliaji: Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Rashid Juma na John Raphael Bocco.