Baada ya habari nyingi kuenea kuwa klabu ya Horoya FC imemsajili kiungo wa Azam FC Tafadzwa Raphael Kutinyu kwa muda wa miaka miwili.
Akiongea na mtandao huu , meneja wa Azam FC, Philip Alando amedai kuwa hawana taarifa ya habari hizo zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii.
“Hata mimi hizi habari naziona kama unavyoziona wewe kwenye mitandao ya kijamii, Kutinyu alituaga kuwa anaenda kwenye kambi ya timu ya taifa ya Zimbabwe”.
” Na mkataba wake unaisha mwishoni mwa mwezi huu, tarehe 30 mwezi huu ndiyo mkataba wake unaisha, lakini habari hizo tunazisikia tu ila sisi hatuna hizo habari rasmi”- alisema meneja huyo wa Azam FC , Philip Alando.