Sambaza....

Ikiwa imesalia miezi kadhaa tu kwa timu ya Tanzania, Taifa Stars kuungana na mataifa mengine  23 katika michuano ya mataifa Afrika AFCON , itakayopigwa kule nchini Misri, Chama cha Soka Afrika, CAF tayari kimejipanga vyema kuhakikisha michuano hiyo inakwenda sawia.

Katika kuhakikisha mashindano hayo yanaendana na maendeleo ya dunia hasa kwa upande wa teknolojia ya mchezo wa mpira wa miguu, CAF wameamua kutumia mfumo wa VAR (Video Assistant Refarees).

Kwa mujibu wa CAF mfumo huo utaanza kutumika kuanzia hatua ya 16 bora.

VAR ni mfumo wa kufanya maamuzi kwa kutazama video za tukio husika. Kuna matukio manne pekee yanayoweza kutaka msaada wa video (VAR)  katika mchezo , nayo ni ;

Goli. Goli likifungwa na likazua utata, hasa kabla ya kufungwa, VAR hutumika kujua kama kuna usahihi wa goli hilo hasa kwa kutazama kama ni Offside au yalitendeka madhambi (Man City vs Tottenham)

Pili, Ni maamuzi ya Penati. Tatu, ni maamuzi ya kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji na nne, VAR hutumika kumbaini mchezaji anayestahili kupewa adhabu, yaani kadi nyekundu au njano.

Baada ya majaribio ya Muda mrefu barani ulaya na duniani kwa ujumla, sasa mfumo huu utatumika barani Afrika katika michuano ya AFCON  2019.

Makocha wengi duniani wanauungamkono mfumo huu, japo kuna wakati huwakosesha raha. Wengine wanadai kuwa, mpira wa miguu kwa sasa umekosa ladha baada ya kubuniwa kwa mfumo huu.

Wewe maoni yako ni yapi juu ya matumizi ya VAR?

Sambaza....