Sambaza....

Kiungo mtaalamu na fundi wa mpira Haruna Niyonzima amerudi tena katika Ligi Kuu Bara, baada ya kulamba donge nono katika usajili wa dirisha dogo.

Nahodha wa Rwanda mwenye mafanikio makubwa katika kunyakua vikombe vya ubingwa wa VPL amerudi tena katika klabu ya Yanga baada kusainiwa akitokea AS Kigali ya kwao Rwanda.

Niyonzima

Haruna Niyonzima amesajiliwa tena na Yanga huku ikionekana wadhamini wa Yanga GSM ndio kwa kiasi kikubwa wakisimamia na kufanikisha usajili huo.

Mpaka sasa Yanga sc imeshatangaza nyota wanne waliowasajili katika dirisha dogo, wakiwemo Ditram Nchimbi, Adeyum Saleh, Haruna Niyonzima na Tariq Seif.

Sambaza....