Sambaza....

Ni rasmi sasa kocha Mholanzi Hans Van Plujim hatokua na kikosi cha Singida utd katika msimu ujao baada ya uongozi wa Singida utd kuthibitisha hilo.

Kocha huyo aliekula amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo ilipopanda daraja mwaka jana amekataa kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuinoa klabu hiyo.

Huku ikisemekana kocha huyo anaelekea AzamFc msimu ujao tayari klabu ya Singida utd imeanza kutafuta mmbadala wake huku Ettiene Ndariagije akipewa nafasi kubwa kuchukua mikoba ya Mholanzi huyo.

Azam fc inatafuta kocha mpya baada ya kocha wake Artística Cioaba kutimka katika timu hiyo hata kabla ya msimu kumalizika. Huku ikisemekana amepata dili kubwa zaidi hivyo kumfanya kuachana na AzamFc.

Ettiene Ndariagije aliekula akiinoa Mbao fc kabla ya kuachana na timu katikati ya raundi ya pili na kurudi kwao Burundi huku nafasi yake ikichukuliwa na Furgency Novaty aliekula katika benchi la timu ya Taifa.

Singida utd tayari wameanzaa mazungumzo na Mrundi huyo ili aweze kukiongoza kikosi hicho katika msimu ujao wa ligi na pia huenda katika michuano ya Kimataifa endapo wataifunga Mtibwa Sugar katika fainali ya Azamsports FederationCup.

Hivyo basi msimu ujao huenda mabenchi ya ufundi ya timu za Azam fc na Singida utd yakawa na sura mpya katika uongozi wao.

Sambaza....