Usiku wa Jana jumamosi ya tarehe 28/05/2022 Dunia ya soka ilishuhudia klabu kongwe ya Real Madrid ikitwaa ubingwa wa UEFA Champion league kwa kuwafunga Liverpool 1-0. Ni kombe lao la 14 la klabu bingwa Ulaya ambalo Waspaniola wanaita La decimocuarto.
Haikuwa game nyepesi kupata matokeo kama ambavyo sifa ya fainali inavyojulikana ni ngumu isiyo na nafasi nyingi za kufunga (Intact).
Binafsi naamini katika uzoefu wa kocha Carlo Ancelotti ndiyo umefanikisha ubingwa huu, mpango wa mechi ( match strategies) ilikuwa ya hali ya juu kwa Real Madrid hasa kwenye kuifanya kutoruhusu bao la mapema katika dakika 45 za kwanza.
Ancelotti alikwenda na 4-3-3 kama ilivyo kwa Jugen Klopp na Liverpool yake.
Hapa mabeki 4 wakiongozwa Dani Alaba na Eder Militao ,Ferlan Mendy na Dan Carvajal ambapo Kocha Ancelotti aliwapunguzia majukumu ya kwenda mbele kuongeza mashambulizi.
Viungo wake ni watu ambao umri umesogea akianza na Luka Modric (36) Toni Kroos (32) na Casemiro 30 ambao kiufundi wapo vizuri ni wasahihi sana wa vitendo hasa kwenye kupiga pasi na kumiliki mpira.
Upande wa ushambuliaji Kocha Carlo Ancelotti aliorodhesha washambukiaji watatu Vinicius aliyekuwa shujaa wa mchezo lakini pia Kareem Benzema na Federico Valverde ambaye ni kiungo ila kwenye mpangilio anacheza kama mshambuliaji lakini jukumu lake Mama ni kucheza kwenye kiungo kuwaongezea nguvu idara ya kiungo yenyewachezaji wengi ‘veterans’.
Hapa Liverpool ndipo walipoingia kwenye mtego kwa kuzidiwa idadi ya viungo badala ya kuwa 3v3 inakuwa 4v3 ndipo game ilipohamia kwao hasa mpango wa kwanza ulivyofanikiwa wa kutoruhusu goli mapema.
Hivyo Thiago Alacantara Fabinho na Captain Jordan Henderson kufichwa au kumezwa kabisa na viungo wa Real Madrid.
Liverpool iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuwa clinical kumalizia.
Licha ya upinzani mkubwa toka kwa golikipa wa Real Madrid Thibath Courtois ambaye alikuwa na siku nzuri sana.
Vinicius Jr alipunguza uwezo wa mlinzi wa pembeni Trent Alexander Anold kutokupanda kuongeza nguvu kwenye mashambulizi the same na upande wa Andy Robertson.
Na kutokana na hofu ya Kareem Benzema kuliwafanya walinzi wa kati Konate na Van Dijk kutokupanda kuongeza nguvu.
Na hivyo wachezaji wa safu ya ushambuliaji kucheza kama’ wapweke’ ambao ni Luiz Diaz ,Mohammed Salah na Sadio Mane
Mechi hii kiukweli imeamriwa na ubora na uzoefu wa benchi la ufundi la Mabingwa Real Madrid chini ya mzoefu Don Carlo ambaye wamewahi kuwapa ubingwa huo mwaka 2014 lakini anahistoria nzuri ya kombe hilo akilitwaa jumla ya mara 4 mwaka 2003 ,2007 2014 na hii 2022.