Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametoa onyo la mapema kwa Yanga kuelekea kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na kuacha kulalamika kwa mamlaka za soka.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Manara amesema Yanga bado wanahangaika na usajili huku wakiwa hawajaanza kambi, pia amewakumbusha Octoba 18 sio mbali kuelekea mchezo wa Watani wa Jadi.
“Tupo mazoezini na kocha wetu Sven yupo, tayari tumeshamaliza usajili wetu wa wachezaji wapya na hakuna mchezaji wa timu ya kwanza aliyeondoka, lakini kwa Yanga theluthi moja ya timu wamefukuzwa. Chondechonde Yanga msije kuwasingizia TFF au bodi ya Ligi kuwa inaisaidia Simba wakati msimu unaanza.” Hajji Manara.
Haji ameongeza “Wenzenu tunajiandaa ila nyie bado mnakatika masebene huko Kalemie Usisahau derby yetu ni tarehe 18 Oktoba, sio mbali, msije kuwatafuta muhali kina Karia.. onhoo Hamkawii kusema Simba TFF Simba, Spika Simba na Waziri Mkuu Simba. Wenzenu tunajiandaa ila nyie bado mnakatika masebene huko Kalemie kuaadanganya watu wenu.
Nawakumbusha Utopolo Simba sio watu ndugu zangu, wanaweza kuwapiga kumi, nawajua walivyokua hawana huruma. Endeleeni tukujitoa ufahamu.”