Baada ya kuonekana Yanga inasua sua kwenye masuala ya uchumi , GSM anaonekana kama mkombozi mkubwa wa klabu hiyo ambapo anafanya usajili katika maeneo ambayo yanaonekana yanahitaji nguvu.
Mpaka sasa hivi GSM wamefanikiwa kumrudisha Lamine Moro ambaye alikuwa amedaiwa kuondoka kutokana na kuidai Yanga fedha ya mshahara wa miezi miwili. Pia GSM wamefanikiwa kumrudisha tena Haruna Niyonzima katika kikosi chao, huku wakimsajili Mshambuliaji Ditram Nchimbi.
Kufuru inazidi kuwa kubwa maana kuna tetesi kuwa kocha wa zamani wa Simba , Patrick Aussems yuko kwenye mazungumzo na GSM ili kuwaza kurudi kwenye klabu hiyo. Kama akifanikiwa basi anakutana na timu yake ya zamani Simba. Yanga mpaka sasa hivi iko chini ya kocha wa muda Charles Boniface Mkwasa.